Serikali
imesema kuwa Tanzania haiwezi kubadirika ikiwa mawazo ya watu
hayatabadirika katika ujenzi wa viwanda vidogo nchini kote na kuondoa
mawazo ya kujenga viwanda vikubwa kama vya wafanyanyabiashara wakubwa,
kwa kuwa vinahitaji mtaji mkubwa wakati ajira zake ni chache.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa
Seleman Jaffo alitoa kauli hiyo tarehe 22 Decemba, 2015 wakati
alipotembelea taasisi zilizo chini ya Wizara yake ambazo ni LAPF na
Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa zilizopo mjini Dodoma.
Alisema
baadhi ya Watanzania wamekuwa na mawazo kuwa viwanda vikubwa ndiyo
vyenye ajira nyingi wakati viwanda hivyo kwa sehemu kubwa vinatumia
mashine wakati viwanda vidogo ndiyo vyenye uwezo wa kutoa ajira kwa watu
wa kada ya chini kwa wingi.
Naibu
Waziri alitolea mfano wa nchi za China na India kuwa wananchi wao
wamewekeza katika viwanda hadi vipo viwanda vya familia na maisha
yanasonga kwa ubora mkubwa kuliko maeneo mengine ya dunia.
“Watu
wanaamini kazi kubwa ni kujenga viwanda, Mheshimiwa Rais anataka
viwanda vijengwe kwa wingi na hata chumba cha nyumba kinatosha kuwa ni
kiwanda kidogo cha kufanya kazi yoyote na mtu akapata ajira, kwa hiyo
wakati tunasubiri uwekezaji mkubwa, naomba tuanze na hivyo viwanda
vidogo,” alisema Jaffo.
Aliwaagiza
mifuko ya hifadhi ya jamii kuanza kujikita katika ujenzi na upanuzi wa
viwanda vidogo kuliko kung’ang’ania kuwekeza katika majengo makubwa
ambayo alikiri kuwa yanasaidia kuifanya mifuko hiyo ionekane kuwa ni
hai.
Kwa
upande wake Kaimu Katibu wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa Bibi
Apolonia Chagaka, alisema kuwa bodi yao imejidhatiti kwa kiasi kikubwa
na katika maeneo mbalimbali wamewekeza baada ya kuona mtaji wao umekuwa.
Alitaja
baadhi ya maeneo ambayo wamewekeza ni Mbeya katika ukumbi wa Benjamini
Mkapa, Mbinga, Musoma, Lushoto, Moshi, na maeneo mengi ambayo bado
wanaendelea na mchakato wa ujenzi hivi sasa.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa LAPF bwana John Kida alisema kuwa mfuko huo mbali
na kazi kubwa wanazofanya ambazo zinahusiana na fedha, lakini bado
wameendelea kukua na kuongeza mtaji kutoka 450 bilioni hadi kufikia 983
bilioni.
Kida
alitaja changamoto inayokwamisha mifuko mingine ni kitendo cha serikali
kutokulipa madeni makubwa baada ya mifuko kufanya kazi ikiwemo majengo
ya utawala, miundombinu yote iliyofanywa katika Chuo cha Serikali za
Mitaa Hombolo.
0 comments:
Post a Comment