Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ya Mkoani Iringa imeibuka
mshindi wa kwanza kimkoa na kushika nafasi za juu kikanda na kitaifa, kati ya
Halmashauri tano za Mkoa wa Iringa, baada ya kufanya vizuri zaidi wakati wa
mbio za mwenge wa uhuru ulipokimbishwa Mkoani Iringa mnamo mwezi Juni mwaka
huu.
Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri
ya Wilaya ya Mufindi imevitaja baadhi ya vigezo kati ya vigezo 10 vilivyoshindanishwa, kuwa ni pamoja
na miradi yenye maslahi kwa umma iliyozinduliwa wakati wa mbio za mwenge wa
uhuru, uimarishaji wa vikundi vya uzalishaji mali kwa wanawake na vijana.
Vigezo vingine vinavyozingatiwa ni pamoja na mapambano dhidi
ya Malaria, dawa za kulevya, michango ya Mwenge wa uhuru sanjari na mapokezi ya
mwenge wenyewe ulipowasili wilayani Mufindi
Akizunguzia ushindi huo, Mkuuwa wilaya ya Mufindi JOWIKA KASUNGA amewashukuru wakazi wa
Mufindi na wadau wa maendeleo kwa michango yao na akatoa rai ya kundelea
kuuenzi mewenge wa uhuru kama alama na utambulisho wa taifa.
Aidha, taarifa hiyo imezitaja nafasi ilizoshika kuwa ni
ushindi wa kwanza kimkoa, ushindi wa 05 kwa kanda ya kiuchumi yenye zaidi
Halmashauri 36 pamoja na nafasi ya 22 kitaifa ikijumuisha zaidi ya Halmashauri
140.
0 comments:
Post a Comment