RAYMOND MINJA IRINGA
WATU 12 wamefariki dunia na wengine 28 kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mbao.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa o1;30 za mchana katika eneo katika eneo Igeme wilaya ya kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Morogoro Dodoma .
Akizungumza na blog hii Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi (ACP) Piter Kakamba alisema kuwa basi hilo namba T486 mali ya kampuni ya New Force lilikuwa likitoka Dar esalamu kwenda Tunduma
Kamanda Kakamba alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori aina ya scania lenye namba T616 BEF liliokuwa likitokea mkoani Njombe kelelekea jijini Dar esalamu kupasuka tairi la mbele na kuanza kuyumba na hatimayue kugongana ba basi hilo na yote kuanguka kwa pomoja
Alisema kuwa maiti za ajali hiyo zimehifadhiwa katika hospitali ya mkoa Wa Iringa na na baadhi ya majeruhi huku badhi ya wajuruhi wamepelekwa katika hospitali ya Ilula
Alisema kuwa hali za majeruhi wengine ni mbaya na madereva wote wawili wameumia vibaya huku mwingine akiwa amekatika miguu yote miwili
Hata hivyo kakanda Kakamba alishindwa kutaja majina ya walipoteza maisha na majeruhi kutokana na wengine bado wakiwa wanahamishiwa katika hospitali ya mkoa na kuwataka ndugu jamaa na marafiki waliokuwa wakisafri na basi hilo kuja katika hospitali ya mkoa kwa ajili ya kuja
kutambua ndugu zao
Akizungumzia ajali hiyo mmoja wa majeruhi aliyekuwa akitoka Dar kwenda tunduma Maiko Mahenge alisema kuwa walitoka dar wakiwa na mwendo wa kawaida ila walipofika katika eneo hilo waliona lori hilo likiwa linakuja kwa kasi na kisha kuligonga gari lao kwa mbele na kupinduka Mahenge alisema kuwa licha ya lori hilo kupasuka tairi lakini
lilionekana kufeli breki kwa kuwa lilikuwa likimshinda dereva aliyekuwa akihangaika kulisimamisha bila ya mafanikio yoyote
0 comments:
Post a Comment