Miongoni
mwa mambo yanayotikisa duru za vyombo vya habari nchini Tanzania na nje
ya nchi ni kuhusu ukwepaji wa kodi kupitia utoroshwaji wa makonte
kutoka bandari ya Dar es Salaam.
Hadi
sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya makontena 2,500 yalitolewa pasipo
kulipiwa kodi stahiki kutoka bandari ya Dar es Salaam kati ya mwaka 2013
hadi 2015.
Bandari
ni shirika la Umma ambalo kwa muundo wa Serikali liko chini ya Waziri
wa Uchukuzi na kwa taratibu za Bunge linasimamiwa na Kamati ya Bunge ya
Hesabu za Serikali (PAC) ambayo kwa muda huo imekuwa inaongozwa na
Mheshimiwa Zitto Kabwe.
Hata
hivyo pamoja na hoja binafsi nyingi zilizokuwa zinawasilishwa kwenye
meza ya Katibu wa Bunge kuombewa kibali cha kuwasilishwa Bungeni, hakuna
kumbukumbu zinazohusu kuombwa kwa hoja binafsi iliyohusu suala hili
ambalo ni dhahiri limekuwa linaipotezea Serikali mabilioni ya fedha.
Alipokuwa
akihudumu katika serikali ya awamu ya nne kama Waziri wa Uchukuzi,
Mheshimiwa Dk. Mwakyembe alijitutumua kukamata makontena yasiyozidi
kumi.
Hata
hivyo kasi yake ikapungua taratibu na kisha akawa kimya! Aidha,
aliyembadili katika nafasi hiyo, Samwel Sitta aliingia kwa nguvu sana
lakini hakuweza kugusia eneo hilo kama inavyofanyika sasa.
Haijachukua
zaidi ya mwezi mmoja tangu Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani
kupata na kuanza kuzifania kazi taarifa kuhusu uozo uliokuwepo katika
bandari ya Dar es Salaam. Hili linaacha maswali mengi yanayohitaji
majibu.
1.Je,
ilikuwaje watoa taarifa hizi walishindwa kuzifikisha taarifa hizi kwa
wasimamizi wa bandari na mashirika ya umma wa wakati huo wakiwemo
mawaziri Dk. Harrison Mwakyembe, Samwel Sitta na Kabwe Zitto (Mwenyekiti
wa PAC)?
2.Je, inawezekana kuwa walikuwa na taarifa lakini nao walinyamazishwa?
3.Je, kama walinyamazishwa ilikuwa kwa maslahi ya nani?
4.Je, ni mfumo gani ufuatwe ili PAC iweze kuwawakilisha wananchi pasipo shaka katika kuisimamia Serikali?
5.Je,
si wakati muafaka kwa waheshimiwa hawa na wale wanaoendelea kuwemo
katika Bunge la awamu hii ya uongozi, kujitokeza kueleza wanachokifahamu
kuhusu sakata hili na kilichowanyamazisha ili waweze kuaminika tena?
0 comments:
Post a Comment