Diwani wa kata ya
Gangilonga katika halimashauri ya
manispaa yaIringa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dady Igogo amegomea
kupokea posho zinazotolewa na halimashauri hiyo alimaarufu posho ya vikao(
sitting allowance )na badala yake ametaka posho hizokwenda kusaidi watoto
wanaoshi katika mazingira magumu kwenye kata yake
Diwani huyo mdogo
kuliko madiwani wote wa halimashauri hiyo aliyeshiriki pia katika mchakato wa kuwania unaibu Meya na kujitoa nyakati
za mwisho kutokana na kupata nafasi ya kwenda kusoma atakuwa ni diwani wa
kwanza nchini kugomea posho hizo huku wa kwanza kugomea posho ni mbunge wa Singida Magharibi Ndg. Elibariki
Kingu wa CCM
Akizungumza na
waandishi wa habari katika ofisi ya kata ya Gangilonga Igogo alisema kuwa
ameamua kuchukua uamuzi huo ili kusaidia yatima na kuunga mkono ilani ya chama
chake ya uchaguzi wa 2010 na 2015 ya kukataa posho ya kitako au vikao iweze
kufutwa na tayari ameshamuandikia mkurugenzi barua ili posho hizo ziweze
kupelekwa sehemu husika
Alisema kuwa anaamni
udiwani sio kazi ya ajira bali ni kazi ya kuwatumikia wananchi
waliamuamini na moja ya majukumu ya diwani ni kukaa vikao na hasikii fahari
kuchukua posho ambayo kimsingi ni sehemu ya majukumu yake wa kuwatumikia
wananchi
Igogo alisema kuwa
posho ya vikao ni ugonjwa wa ufisadi unaolitafuna taifa kila kukicha hususani
kwa watendaji wa mashirika ya umma,watendaji wa serekali kuu huu na kumpongeza
Raisi John Magufuli kwa kubana matumizi
yasiyokuwa na lazima katika kuhakikisha fedha zinaelekezwa katika miradi ya
maendeleo na siyo katika masuala ya kiutawala katika kulipana posho
Alisema posho za
wabunge zinalingana na bajeti ya sensa ambapo Taifa lilikwenda kukopa baadhi ya
fedha ili kuendeshea zoezi hilo huku wastani wa posho kwa za madiwani na
watendaji katika manispaa ya Iringa kwa mwaka zinauwezo wa kusomesha zaidi ya
wanafunzi 400 wa shule za sekondari kwa ada ya shilingi eflu 20,000#kwa kila
mmoja na fedha zikabaki
Hata hivyo Igogo
aliwaomba madiwani wa chama chake na mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Piter
Msigwa na wabunge wote wa viti maalumu kuwa sehemu ya kupinga uendelezwaji wa
posho zisizo za msingi ili kuonyesha dhamira ya dhati katika kuwatumikia
watanzania
Katika vhatua nyingine
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilaya ya Iringa mjini
ambaye pia ni diwani wa kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi amesema uamuzi
aliochukua diwani huyo ni mzuri na ni maamuzi yake ila yeye hana mpango wa
kugomea kuchukuA posho hizo
Alisema kuwa posho ya
vikao hivyo ni haki yake kama diwa aliyepewa dhamana na wapiga kura wake lakini matumizi yake atayapanga mwenyewena
kuamua kuwa azielekeze wapi fedha hizo
katika kutatua changamoto mbalimbali lakini hayuko tayari kutamka hadharini
kuwa hata chukua posho hizo kwani itakuwa ni kuwahadaa watu
Wakizungumzia uamuzi
huo wakazi wa mjini Iringa Abdulkarimu Rashindi ambaye ni mfanyabiashara na
kusema kuwa uamuzi aliochukua diwani huyo ni wa kishujaa na kuigwa kwani watimishi
wengi wa serekali wamekuwa wakilipana posho za vikao hata ambavyo havina msingi
wowote
‘’Asee mi naona
wapinzani nao wanaanza kufuata nyao za Raisi wangu Magufuli kwa kuwa mzee naye
alisema hizi posho posho hakuna mana watui walikuwa wanajipigia helaa tuu yani
watu wanatoka Iringa wanaamua tuu kwenda kuafanyia kikao mbeya ili poshoo iwe
kubwa sasa imekula kwao wamebanwa kila kona huyo dogo naye kafanya vema na
wengine wanapaswa kuiga ‘’
Alisema masauala ya
vikao ni majukumu ya kawaida kwa watendaji na wabunge hivyo swala la posho siyo
la lazima kwa kuwa watu hao wanalipwa mshahara na wengine posho za mwezi hivyo
masuala ya posho yapigwe marufuku na fedha hizo zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo
0 comments:
Post a Comment