Baada ya kuwa kimya tangu ashinde
Ubunge, Mbunge wa Kibamba kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika ameibukia
kwenye sakata la ubadhirifu kwenye Mamlaka ya Bandari nchini na kuitaka
serikali kuweka wazi ripoti za Dk. Harrison Mwakyembe na Samwel Sitta.
Mnyika ameyasema hayo jana alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amedai kuwa
ripoti za Sitta na Dk. Mwakyembe zimebeba ukweli zaidi kuhusu
kinachoendelea bandarini hivyo kuziweka wazi kutasaidia kutibu tatizo
lililopo zaidi ya kuwasimamisha watendaji waliotajwa.
Akiyafananisha matatizo ya bandari na
majipu anayoyatumbua rais John Magufuli, alisema kuwa dawa yake ni
kuyapasua ili kuondoa kiini badala ya kuyatumbua tu.
“Dawa ya jipu sio kulitumbua bali ni
kulipasua ili kiini cha ndani kitoke, ukikiacha jipu linaazna upya tena
linakuwa hatari zaidi,” alisema Mnyika.
“Kama kweli serikali ya awamu ya tano
ina lengo la kufichua ufisadi, basi inapaswa kuweka wazi ripoti
mbalimbali za uchunguzi ziwe dira ya kujua kiini cha matatizo kujitokeza
katika Mamlaka ya Bandari,” aliongeza
0 comments:
Post a Comment