Pichani Mbunge wa jimbo la Mafinga mji ni
Cotato chumi akimkabidhi msaada
wa vitanda ,magodoro pamoja na vifaa mbalimbali kaimu mganga mkuu wa
hospitali ya Mafinga dk Abdul Msuya juzi
baadhi ya waandishi wa habari wakifuatiliwa ugawaji wa vifaa hivyo wakati wa makabidhianombunge wa mafinga mjini cosato chumi akikabidhi vifaa hivyo kwa vitendo
baadhi ya wadau na wanachama wa chama cha mapinduzi ccm walihudhulia tukio hilo
TATIZO la upungufu wa vitanda katika wodi ya
akina mama na watoto katika hospitali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
ambalo kwa muda mrefu limekuwa chanzo cha msongamano na uwalazimu
baadhi ya wagonjwa kulala sakafuni sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya
uongozi wa hospitali hiyo kupokea msaada wa vitanda na vifaa tiba kutoka
kwa mdau wa maendeleo katika sekta ya afya.
mbunge wa Mafinga Mjini
(CCM) Cosato Chumi alisema kuwa kwa muda mrefu hospitali hiyo ilikuwa ina
upungufu wa vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda hali iliyofanya kuandika maandiko
mbalimbali kwa wahisani wa nje ya nchi ili kuweza kumsaidia kupata
vifaa hivyo .
Alisema kuwa umefika
wakati sasa wadau mbalimbali, mifuko ya kijamii na makampuni kujenga utamaduni
wa kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo watoto wanaoishi kwenye
mazingira magumu na wagonjwa hospitalini kwani kufanya hivyo ni sehemu ya
kurudisha kile wanachokitapa kwa jamii.
“Unajua afya ni kila
kitu katika maisha ya binadamu hivyo lazima nitekeleze ahadi zangu nilizotoa
wakati wa kampeni na wanachi lazima tufanye kazi kwa kujituma ili tumuunge
mkono rais wetu ambaye anania ya ya kutuletea maendeleo na kuwataka wadau
mbalimbali kusaidia jamii zenye mahitaji na kuacha kutegemea serikali pekee “
alisema
Chumi aliwaomba wananchi
wa jimbo hilo kuunga mkono kwa kufanya kazi kwa nguvu zote ili walete maendeleo
kwa pamoja maana akifanya kazi pekee yake bila wao hawezi kuleta maendeleo
pekee yake.
Msaada huo wa vitanda 16 na magodoro 11 na vitu
mbalimbali umetolewa na taasisi binafsi inayojishughulisha na masuala ya
afya ya nchini Astralia ijulikanayo kama “Rafiki Surgical Mission” kwa
uratibu wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Mafinga mjini
“Ndugu zangu nadhani kila mmoja alikuwa akifahamu machungu waliyokuwa wakipata mama zetu wanapokuja kujifungua kwa kukosa sehemu za kujifungulia lakini leo hii msaada huu utatusaidia sana na yoyote atakayeguswa na anaweza kuja na kuchangia chochote maana mufindi ni yetu sote na mufindi itajegwa na wanamufindi wenyewe”alisema
Alisema jambo kubwa lilokuwa likimuumiza kicha kila kukicha ni tatizo la vifaa katika hospital, elimu pamoja na tatizo la maji hivyo ni wakati wawanamafinga kushikana kwa pamoja katika kusumkuma mbele gurudumu la maendeleo ili kuendana na kauli mbiu ya sasa ya HAPA NI KAZI TU.
Akipokea msaada huo kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga dk Abdul Msuya alisema kuwa msaada wa vitanda hivyo na magodoro na vifaa mbalimbali utakuwa umemaliza kabisa tatizo la vitanda hospitalini hapo licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kumalizika endapo kutatokea mdau mwingine kuwasaidi Kwa upande wake katibu wa ccm wilaya ya Mufindi Jimsoni Muhagama
alimpongeza mbunge huyo kwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo huku akimwambia kuwa ni wakati wa kutekeleza kazi kwa vitendo na wala si maneno kwani wananchi wanapaswa kutatuliwa kero mbalimbali zinazowakabili badala ya kupiga porojo zisizo na msingi .
Mhagama alisema kuwa kila mmoja anapaswa kuwajibika ipasavyo katika nafasi yake kwani kasi anayokwenda nayo Rais John Magufuli si ya mchezo bali ni ya mchaka mchaka na ili nchi iweze kusimama katika mstari ulionyoka kila mmoja anapaswa kucheza wimbo wa mchaka mchaka
‘’Huuu si wakati lelemama huu sio wakati mchezo mchezo ni wakati wa uwajibikaji ,hakika Tanzania tumepata kiongozi mchapa kazi tazama sasa ni siku ya 27 nchi inaongozwa na watu wanne lakini kila sektaa imenyoka na mimi nasemaa Magufuli wanyooshe tu kwa kuwa watu walikuwa wakifanya kazi kwa mazoeya bila ya kuangalia madhara wanayopata
watanzania swengi
Hata hivyo Mhgama alisema kuwa kwa kuwa kipindi cha muda mchache nchi inaongozwa na watu wachache na nchi imesimama haoni sababu ya kuwa na baraza kubwa la mawaziri bali Rais Magufuli achague baraza dogo kama
la watu 10 ili kupunguza mzigo kwa serekali yake ya kuwa na mawziri wengi wasiokuwa na tija .
0 comments:
Post a Comment