Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia
heri watanzania wote katika siku ya UKIMWI duniani itakayofanyika kesho
tarehe 01 Desemba, 2015
Katika
salamu hizo Rais Magufuli amesema jukumu la kupamana na UKIMWI
linamhusu kila mtu na hivyo amewasihi watanzania kuzingatia mahubiri ya
viongozi wa dini, na pia kuzingatia elimu itolewayo na wataalamu wa afya
katika kujikinga na ugonjwa huo.
Dkt.
Magufuli amewahakikishia waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI kuwa Serikali
itaendelea kuimarisha tiba na huduma zao na ndio maana alielekeza fedha
zote zilizopatikana kwa kufuta shamrashamra za maadhimisho hayo
zielekezwe kununulia dawa za kurefusha maisha kwa wagonjwa wa UKIMWI.
Rais
Magufuli ameahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa elimu kwa umma juu ya
kuepukana na maambukizi mapya na kuhimiza watu kujitokeza kwa hiari
kupima afya zao.
Amewaomba
viongozi katika ngazi zote kuendelea kuwahimiza akinamama wajawazito
kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kuchunguza afya zao ili
wale ambao watakaogundulika kuathirika na ugonjwa huo, wapatiwe dawa za
kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Aidha,
Rais amewapongeza wadau wa ndani na nje ya nchi wanaoshirikiana na
Serikali katika kupambana na janga la UKIMWI na kuwaomba wadau hawa wa
maendeleo kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
30 Novemba, 2015
0 comments:
Post a Comment