Wananchi wa manispaa
ya iringa wametakiwa kujitokeza kufanya usafi wa mazingira siku ya leo kwa
lengo la kumuunga mkono rais wa jamhuri ya muungano dr john pombe magufuli.
Akizungumza na
waandishi wa habari katibu wa ccm wilaya ya iringa Elisha mwampashe amewaomba
wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya usafi katika maeneo yao.
Aidha mwampashe
amewataka wananchama wa chama hicho kufanya usafi kwa kujituma na kuwaomba
manispaa kutunga sheria elikezi za utupaji wa takataka ili kutimiza wazo la
rais wa chama hicho cha kufanya kazi.
“wananchi wa manispaa
ya iringa mjitokeze kwa wingi tufanye usafi kwa kujituma na zoezi hili liwe
endelevu kwa kuwa kufanya usafi ni jadi yetu sio lazima rais atoe tamko lazima
wananchi wenyewe tujitafakari “alisema mwampashe.
Mwampashe alimalizia
kwa kuwataka viongozi wa manispaa kutoa ushirikiano kwa wananchi ili kuufanya mji wa iringa kuwa msafi kila
kona na kutunga sheria zitakazokuwa zikimbana mwananchi asichafue miji.
0 comments:
Post a Comment