WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewaonya watendaji wa halmashauri nchini kwamba
atakayebainika ametumia vibaya fedha za Serikali atang’olewa kazini kwa
sababu Serikali ya Awamu ya Tano haina mchezo na mtu.
Alitoa
kauli hiyo jana mchana (Jumapili, Desemba 20, 2015) wakati akizungumza
na mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu uliopo Lindi mjini.
“Natoa
onyo kwa watendaji wote wa halmashauri. Fedha ya Serikali itakayotumwa
kwenu halafu mtu aifanyie ubadhirifu, ole wake. Yeyote atakayebainika
kuzitumia kwa ubadhirifu fedha hizi tutamng’oa. Wako wasomi wengi huko
nje tena wazuri tu, wanasubiri kupata ajira.”
“Nataka
watumishi wa umma watambue kwamba Serikali ya Awamu ya Tano
inajielekeza kujali wananchi. Wao wana dhamana ya kuwasilikiliza na
kuwahudumia wananchi ili kuhakikisha wanatatua kero zinazowakabili, ”
alisema huku akishangiliwa na wengine wakisema huyu sasa ni Sokoine wa
pili. (Edward Moringe Sokoine alikuwa ni Waziri Mkuu katika Serikali ya
Awamu ya Kwanza).
Waziri
Mkuu ambaye aliwasili Lindi Jana, aliwaeleza wakazi hao kwamba amekuja
kuwashukuru wazee na wana Lindi kwa dua zao na kuwaahidi kwamba
hatawaangusha Rais John Pombe Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu
Hassan kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kuwatumikia Watanzania katika
ngazi ya Uwaziri Mkuu.
Waziri
Mkuu pia alimpa kazi Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Jordan Rugimbana ya
kuhakikisha anaufufua uwanja huo na kuurudisha kwenye enzi yake
ulivyokuwa maarufu katika mikoa yote ya Kusini.
“Uwanja
huu lazima uboreshwe kwa sababu unanikumbusha mwaka 1984 wakati
nachezea timu ya Amri Rangers. Kulikuwa na ukoka wa nguvu hapa
uwanjani. Kwa hiyo timu aliyoiunda Mkuu wa Mkoa itafanya kazi lakini pia
iwajumuishe Meya na mbunge wa Lindi Mjini kwa sababu huu uwanja ni mali
ya Halmashauri ya Lindi, ” alisema.
Akielezea kuhusu mipango ya Serikali kuendeleza sekta ya viwanda, Waziri Mkuu alisema hivi karibuni mkoa huo utapata wawekezaji kwenye sekta ya gesi baada ya kampuni ya BG kutoka Uingereza kupata umiliki wa eneo la Kikwetu ili wajenge mitambo ya kusafisha gesi.
Aliwataka wananchi wa mkoa huo wawekeze kwenye ujenzi wa hoteli na nyumba za kulala wageni ili ifikapo Agosti mwakani, watu wanaokuja kushiriki maonyesho ya NaneNane kitaifa mkoani humo wasipate taabu ya malazi kama ambavyo imekuwa ikitokea huko nyuma

0 comments:
Post a Comment