Madiwani kumi wa Chama Cha wananchi
(CUF) waliodaiwa kufanya vurugu katika uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya
jiji la Tanga wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Hayo yalisemwa jana na Kamanda wa Polisi
wa Tanga, Zubery Mwombeji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu tukio la vurugu zilizotokana na madiwani wa CUF kupinga matokeo
ya uchauguzi huo.
Kamanda Mwombeji alisema kuwa madiwani
hao walikamatwa na kupelekwa katika kituo cha Polisi cha Chumbageni na
baadaye waliachiwa kwa dhamana majira ya saa sita usiku.
Alisema kuwa madiwani hao walikamatwa
kwa tuhuma za kufanya vurugu na kuchoma pazia na kujaribu kuvunja mlango
wa ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo.
Madiwani wa CUF wanadaiwa kufanya vurugu
katika ukumbi wa halmashauri ya jiji hilo uliotumika kupigia kura baada
ya Mkurugenzi wa jiji hilo kumtangaza diwani wa CCM, Mohamed Mustafa
kuwa mshindi kwa kupata kura 19 dhidi ya mgombea wa CUF aliyepata kura
18.
CUF walipinga matokeo hayo na kudai kuwa
walihujumiwa na kuporwa ushindi hususan kwa kuwa wana idadi ya madiwani
20 dhidi ya madiwani 17 wa CCM.
0 comments:
Post a Comment