alex kimbe meya na naibu meya joseph lyata
zile ndoto za wafanyabiasha
wadogowadogo kufanya mnada katika eneo la mashine tatu bado halina ufumbuzi
kutoka na eneo hilo kugeuzwa kuwa eneo la kushushia na kupakia abiria wa
daldala za kutoka kihesa kuelekea zizi la ng’ombe na isakalilo.
Hivyo tunaweza kusema kuwa
eneo hilo sasa haliwezi kutumika tena kwa kuweka mnada kwa kuwa muda mwingi
patakuwa panatumika kwa shuguli za daladala.
Wakizungumza na blog hii
baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo wamesema kuwa wamewachagua madiwani
wengi wa chadema pamoja mbunge na kuwapa
halmashauri lakini hawaoni dalili zozote zile za kuwasaidia wananchi kupewa
kibali maalumu cha kufanya mnada katika eneo hilo la mashine tatu angalau mara
moja kwa wiki.
“Angalia mwandishi wahabari wameingia
tu madarakani wametusahau tuliowaweka
hapo maana hatuoni juhudi wala hawatupi majibu yoyote yale juu ya lini tunaanza
kufanya mnada katika eneo” walisema wananchi
Aidha wananchi hao wamesema
kuwa eneo hilo limegeuzwa kuwa vituo vya daladala hivyo nafasi ya kufanya mnada
katika eneo hilo ni gumu mno kutokana na wingi wa daladala ambazo zimehamishiwa
katika eneo hilo.
Kwa upande wake naibu meya JOSEPH
LYATA amesema kuwa wapo kwenye mchakato wa kulitafutia ufumbuzi kwa kuangalia
mpangilio wa mji kwa ofisi ya mipango miji ili kujua eneo hilo linatumika kwa
nini.
“Ziwezi kuamka asubuhi nikawaruhusu wafanyabiasha waanze
kufanyabiasha katika eneo hilo mimi sio mungu kila kitu kinapangwa na mipango miji
kwa hiyo tunaanda mpango sahihi wa maalumu kwa kuwanufaisha wananchi katika
eneo hilo” alisema LYATA
Lakini LYATA amesema kwa
sasa wapo kwenye vikao vya kulitafutia ufumbuzi wa eneo hilo na mambo mengine.
“Tunaomba wananchi wawe na
subira wakati tunatafuta njia mbadala ya lini wanaanza kufanya biashara na
akinani wanatakiwa kufanya biashara sio kila mfanyabiashara atauruhusiwa
kufanya biashara katia eneo hilo”alisema LYATA.
kwa sasa eneo hilo linatumika kushushia abiria na kupakia abiria wa daladala zitokazo kihesa kuelekea isakalilo na zizi la ng'ombe,hapo sasa wananchi na wafanyabiashara ilatakiwa kutafuta njia nyingine ya kufanya biashara kwa sasa
0 comments:
Post a Comment