Mkuu
wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima, ameagiza kuwa mtu yeyote
atakayeugua ugonjwa wa kipindupindu akitibiwa na kupona, atafikishwa
mahakamani kujibu kosa la kukiuka taratibu za afya na kuugua ugonjwa
huo.
Mwamlima alitoa agizo hilo juzi
wakati wa uzinduzi wa usafi wa mazingira na upandaji miti uliofanyika
eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani Manispaa ya Mpanda
mkoani Katavi.
Alisema
yeyote atakayeugua ugonjwa wa kipindupindu wilayani Mpanda, atapatiwa
matibabu, lakini akishapona, atashtakiwa kwa kukiuka kanuni za usafi.
Mwamlima alisema ugonjwa wa kipindupindu husababishwa na uchafu, hivyo kama mazingira ni masafi, mtu hataugua maradhi hayo.
Aliongeza kuwa wajibu wa kila mtu kuishi kwenye mazingira safi na kuuchukia uchafu ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.
Mkuu
huyo wa Wilaya amepiga marufuku baa kufunguliwa muda wa kazi na
kucheza bao na watu kushinda kwenye vijiwe vinavyouza kahawa.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Ibrahim Msengi, amewaagiza
wananchi wa manispaa hiyo kuhakikisha maeneo yao ya kuishi na
wanayofanyia shughuli za biashara yanakuwa katika hali ya usafi.
Alisema
kila Jumamosi wananchi wa manispaa hiyo wahakikishe siku hiyo
wanaitumia kufanya usafi kwenye mitaa yao na kwa Jumamosi ya kwanza ya
mwezi, itakuwa inatumika kwa ajili ya manispaa nzima ya Mpanda
0 comments:
Post a Comment