Thursday, December 10, 2015

TAMASHA KUBWA LA MSAFARA LINALOWAHUSISHA VIJANA KUFANYIKA JUMAMOSI HII IFAKARA MOROGORO.

 
Kutoka kushoto ni Manoah William Waziri wa Elimu Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Agnes Inocent wa YFF, James Isdore Mwenyekiti wa Msafara,Fadhiri Meta kutoka Youth can na  Batseba Modest kutoka Ngao youth wakiongea katika mkutano huo na waandishi wa Habari leo 9.12.2015

 James Isdore Mwenyekiti wa Msafara akizungumzia Shughuli ya msafa kwa ujumla
 Fadhiri Meta kutoka Youth can akizungumzia jinsi Msafara ulivyopokelewa vizuri na mpaka sasa wamepata zaidi ya vijana 500 ambao wanajifunza ujasiliamali na kuibua vipaji na ubunifu mbalimbali.
 Agnes Inocent akizungumzia jinsi watakavyo hamasisha wanawake wengine kujitambua na kuwa wanaweza.
 Batseba Kassanga (Kulia) akitoa wito kwa vijana namna wanavyoweza kujikomboa kupitia Msafara
 Noah William akifafanua jambo kuhusiana na Msafara
Mkutano ukiendelea 

Programu ya Msafara inayoendeshwa asasi tano za kiraia ambazo ni; YouthCAN, TYDC, DARUSO, NGAO YOUTH na Young Feminist Forum kwa uratibu wa Shirika la Oxfam, inatarajiwa kufanyika mapema kesho kutwa katika Mkoa wa  Morogoro wilayani Ifakara.


Programu inayolenga kuwahamasisha vijana kubuni njia za kujikwamua kiuchumi kupitia wenzao waliofanikiwa, itafanyika kwa njia ya tamasha kubwa katika eneo la Uwanja wa Taifa, Ifakara mkoani Morogoro ambapo ndani ya tamasha hilo mitaji na motisha ya kukabidhiwa vitendea kazi itagaiwa kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 24.


Mbali na kutoa elimu na motisha hiyo, tamasha hilo litapambwa na burudani za aina mbalimbali huku pia kukiwa na vijana waliofanikiwa watakao wahamasisha wenzao kupitia kauli mbiu ya Inspire, Aspire and Activate.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More