Mkurugenzi wa
Miradi wa Tacosode, Theofrida Kapinga akizungumza jambo wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa valentine mkoani Iringa
Afisa
mchechemzi wa mradi Abrahm Kimuli akiendelea kutoa elimu kwa wanasemina walikuwa wamehudhuria katika ukumbi wa valentine
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mijadala ya sekta ya afya na jinsi gani wanaweza kutatua changamoto zinazoweza kuikoa sekta ya afya hapa nchini
Na Fredy Mgunda,Iringa.
BARAZA la Vyama vya hiari na
Maendeleo ya Jamii (TACOSODE) limesema wananchi wamekuwa na uelewa kuhamasisha
bajeti kuwa na kipaumbele kwa changamoto zinazowakabili.
Hayo ameyasema Mkurugenzi wa
Miradi wa Tacosode, Theofrida Kapinga wakati akizungumza semina ya kujadilia
jinsi gani ya kutatua changamoto zinazoikumba sekta ya afya iliyofanyika katika
ukumbu wa valentine Manispaa ya Iringa.
“Unajua zamani wananchi hata
viongozi wa sekta ya afya walikuwa wagumu kuelezea changamoto zinazowakabili
lakini saizi wananchi na viongozi wamekuwa na elimu ya kutosha juu ya kueleza
changamoto zilizopo katika sekta hiyo ndio maana vitu vingi vinaibuka muda huu”
alisema Kapinga
Kapinga alisema licha ya
serikali kufanya juhudi kutatua changamoto ili kuto huduma ya afya bora lakini
bado sekta hiyo inaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo
zinakwamisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.
“Ukiangalia tafiti nyingi
zinaonyesha kuwa serikali imekuwa ikishindwa kuongeza bajeti ya sekta ya afya
ili kufikia asilimia 15 ya bajeti yote ya serikali kwa kuzingatia azimio la Abuja”
alisema Kapinga
Aidha kapinga alisema kuwa
moja ya changamoto kubwa ni uhaba wa kupatikana kwa dawa muhimu,vitendanish na
vifaa tiba kulinganisha na utafiti wa mwaka 2012 ulifanywa na taasisi ya afya
ya Ifakarana kugundua kuwa asilimia 41 ya dawa muhimu zinahitajika kwa kiasi
kikubwa.
Kwa upande wake afisa
mchechemzi wa mradi Abrahm Kimuli aliwataka watumishi wa sekta ya afya
kuzibaini changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi kushirikiana na
serikali panoja na sekta binafsi.
“Unajua kweli kuna changamoto
nyingi ambazo zinawakabili hivyo ni lazima muwe wabunifu kuzitafutia ufumbuzi
lakini kwenye hizi sekta binafsi kuwa wasomi wengi ambao wanaweza kutoa ushauri
mzuri wa kutatua changamoto zilizopo” alisema Kimuli
Kimuli alisema kuwa wananchi
wamekuwa na uelewa wa maswala ya afya kutokana na elimu waliopata katika mradi
wa uhamasishaji wananchi kushiriki katika masuala ya afya katika kuangalia
vipaumbele vya bajeti uliokuwa ukitekelezwa katika Mikoa ya Iringa pamoja na
Dodoma.
Alisema kuwa wananchi mradi
huo katika utekezwaji wake katika Halmashauri ya Iringa pamoja na Kongwa mkoani
Dodoma wananchi wamekuwa na mwamko katika masuala ya afya ushiriki kwa
kuchangia katika huduma za afya.
Kimuli alisema kuwa mradi
huo wa miaka minne umekuwa na matokeo katika wilaya ambazo umetekelezwa kwa
wananchi kuwa na mwamko katika masuala ya huduma za afya kwa kuchangia hata
nguvu zao pale panapobidi.
Aidha amesema kuwa mradi huo
ukiisha wanaweza kufanya katika sekta zingine ili kuwa maendeleo ya katika
masuala mbalimbali kutatuliwa.
Akizungumza kwa niaba ya
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Abel Mgimwa alisema kuwa serikali
ya awamu ya tano imejipanga kuahakikisha changamoto zinatatuliwa kimkakati
kulinga na bajeti wanayokuwa wameipanga.
“Ukiangalia bajeti ya mwaka
wa fedha mwaka huu imepanda hivyo ni dalili njema za kuanza kutatua changamoto
ambazo zimekuwa zikidumu kwa miaka mingi na kuwaomba wananchi na viongozi kuwa
na subira katika kipindi hiki cha utatuzi wa changamoto hizo” alisema Mgimwa
Mgimwa aliwapongeza TACOSODE
kwa mchango wao katika sekta ya afya ambayo imekuwa na changamoto nyingi hivyo
sio rahisi kwa serikali kutatua kwa haraka hivyo.
0 comments:
Post a Comment