Friday, October 6, 2017

MKAZI WA KATA NA KIJIJI CHA BUKONDO WILAYANI GEITA AMEFARIKI BAADA YA KUSHAMBULIWA NA MAMBA.

Kichaka ambacho kipo ndani ya ziwa Viktoria na baadhi ya mitumbwi ya wavuvi ambacho ndicho kinasadikika mamba huyo upenda kujificha kwenye maeneo hayo.

Ramadhan Dadila ni moja kati ya watu ambao walikuwa na marehemu hapa anazungumza na waandishi wa habari namna ambavyo waliachana  wakati wakiwa kwenye shughuli za uvuvi.

Afisa mtendaji wa Kijiji hicho Bw,Beatus Mazezele akielezea namna ambavyo walipatiwa taarifa ya mtu huyo kushambuliwa na mamba .

Wanakijiji wakiwa wamekusanyika kando kando ya vikwe wakisubilia kuanza kumuwinda Mamba .





PICHA NA JOEL MADUKA. 







Mkazi   wa Kata   na kijiji cha  Bukondo   Wilayani Geita  Bw  Yusufu Samson  amemezwa  na mamba wakati  akiwa katika  shughuli  zake  za uvuvi  Oktoba  2.


Maduka Online  imefika Kijijini Hapo na kuzungumza na Baadhi ya  watu ambao alikuwa nao katika shughuli hiyo  ya uvuvi ambapo  wameelezea  hali  ilivyokuwa na  hadi  umauti  ulipomkuta,  John Katamla  na Ramadhan Dadila,wameelezea kuwa  walikuwa  naye  wakati  wa shughuli  za  kuloa  samaki lakini hata hivyo hali haikuwa  nzuri  hivyo  ilibidi  wakunje ndoano kwa  ajili ya kurudi Nyumbani ingawa  marehemu  alikuwa  anaendelea  kuvuta  kamba   za  nanga.

Mwenyekiti  wa Kijiji  hicho   MAKOYE  SOJINGWANONI   amethibitisha kutokea  kwa tukio hilo ambapo  amesema  asubuhi wamemwona mamba huyo akitembea maeneo hayo lakini  hawakuweza  kumfanya lolote  hivyo wameomba msaada  kutoka  kwa  mali asili.

Mtendaji wa Kijiji cha Nyansalala,Bw Beatus Mazezele  amesema  tukio la kukamatwa na mamba mtu sio la mara ya  kwanza kwani yamekuwa ya kijirudia mara kwa mara   hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuachana na dhana ya kuendelea kuogelea  maeneo  ya  ziwani.

Afisa  wanyamapori  wa Halmashauri  ya Wilaya ya Geita Msese  Msese amesema  hadi kufikia  siku  ya jana walipata baadhi ya vipade vya mwili na  bado wanaendelea na jitihada ya kuutafuta mwili huo pamoja na mamba  ambaye amekuwa ni tishio kwa wananchi wa maeneo hayo.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More