Wednesday, January 17, 2018

PICHA ZA MATUKIO YA KUUNGUA KWA NYUMBA ANAYOKAA KATIBU WA UVCCM ALPHONCE PATRICK MUYINGA

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas akizunguza na waandishi wa habari katika eneo latukio huku akiwa anasikitika kwa kilichotoa kwa katibu wa UVCCM 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa bwana CHRISTOPHER MAGALA na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM Mkoa wa Iringa SALIM ASASI wameomba kufanyika kwa uchunguzi wa tukio hilo kwani huenda likawa limehusishwa na Siasa.
mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoani iringa akiwa na uongozi wa mkoaw wa vijana hao wakilaani tukio lilomtokea katibu wa vijana wa wilaya ya Iringa Mjini
Katibu wa UVCCM MUYINGA, amesema moto huo ulianzia katika chumba chake ambapo wakati akiwa amelala alisikia dirisha lake likivunjwa na kuhisi kitu kimerushwa ndani mwake na baadaye moto kuripuka.
Mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoani iringa akiwa na uongozi wa mkoaw wa vijana hao wakilaani tukio lilomtokea katibu wa vijana wa wilaya ya Iringa Mjini akiwa katika eneo la tukio ambapo kila kitu kimewaka moto hivyo na kumuacha katibu huyo kutokuwa na makazi ya kudumu hivi sasa 
Baadhi ya mali ambazo zimehalibiwa na moto huo ulitokea amjira ya saa sita usiku au saa saba hivi
Katibu wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa Mjini Bw. ALPHONCE PATRICK MUYINGA akiwa na katibu wa vijana mkoa wa Iringa Mgego


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Nyumba moja iliyopo kata ya Kihesa Manispaa ya Iringa anayoishi Katibu wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Mjini Bw. ALPHONCE PATRICK MUYINGA imeteketea kwa moto huku chanzo hakijafahamika .

Akizungumzia Chanzo cha moto huo Katibu wa UVCCM MUYINGA, amesema moto huo ulianzia katika chumba chake ambapo wakati akiwa amelala alisikia dirisha lake likivunjwa na kuhisi kitu kimerushwa ndani mwake na baadaye moto kuripuka.

Nao waathirika wa janga hilo ambao ni wapangaji wa nyumba hiyo na wachache wao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa(Tumaini)  wamesema katika ajali hiyo vitu vyote vimeteketea kwa moto na hakuna vitu walivyofanikiwa kuviokoa.

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa bwana CHRISTOPHER MAGALA na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM Mkoa wa Iringa SALIM ASASI wameomba kufanyika kwa uchunguzi wa tukio hilo kwani huenda likawa limehusishwa na Siasa.

Akithibitisha kutokea kwa moto huo Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto Mkoani Iringa Kamanda JAMES JOHN amesema wanaendelea na uchunguzi wa chanzo cha moto huo.

Huu ni mfululizo wa matukio kwa wanasiasa Mkoani hapa ambapo hivi karibuni aliyekuwa Diwani wa kata ya Mwangata alibolewa nyumba yake eneo la Igumbilo Manispaa ya Iringa

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More