Thursday, April 5, 2018

Tagoane na CRDB kuwezesha wasanii

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.
Mtandao wa Wasanii wa Tasnia ya Injili na Maadili ya Utaifa (TAGOANE) kwa kushirikiana na Benki ya CRDB wameanza mchakato wa kuwainua wasanii kiuchumi kupitia mfuko wa akiba unaoitwa Tagoan Loan Fund.
Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa Tagoane Dk Godwin Maimu Nnyaka alisema wasanii wataweza kunufaika na mfuko huo, kwa kuweka na kukopa fedha.
“Kupitia mfuko huo, wasanii na wadau wa tasnia hiyo wataweza kuunga mkono na kuingia moja kwa moja kwa vitendo katika kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya Viwanda. Ili kuhakikisha Mfuko huu unafanya vizuri, TAGOANE inatumia mfumo wa kisasa wa ‘SIM ACCOUNT’ yaCRDB BANK,” alisema..
Alieleza kuwa lengo kubwa la Tagoane kuanzisha mfuko huo ni kuwaunganisha wasanii na wadau wa tasnia hiyo ili kujikwamua kiuchumi.
“Jambo la kwanza kabisa, msanii atapaswa kuwa na simu yoyote ya mkononi, inayotumia mtandao wowote ili kujisajili na simu akaunti kwa kupiga *150*62# kisha unabofya OK kisha unakuta unajisajili. Baada ya hapo, msanii anapaswa kufika kwenye tawi lolote na Bank ya CRDB au kwa wakala ‘Fahari huduma’ kuukamilisha usajili huo,” alisema Dk Maimu..
Alisema hapo msanii ataweza kutumia simu akaunti, kuweka fedha kwa matumizi yake binafsi na kutuma kwenye akaunti ya Tagoane Loan Fund kupitia mfumo huo wa digitali. Kwanini Tagoane tumechagua mfumo huu, moja kwa sababu ni salama na msanii mwanachama ataweza kuona kinachoendelea na kudhibiti matumizi yoyote ya fedha.
 “Wasanii ni kati ya watu wasionufaika na kazi zao, hawana dhamana ya mikopo na kwa kweli wengi wao hawakopesheki. Hii ilisababisha tuungane na tuanzishe mtandao wetu ambao leo hii tunafurahi kuona kwamba tayari tunao mfuko wetu wa mikopo ambao wataweza kuutumia katika kujikwamua kiuchumi,” alisema Rais wa TAGOANE, Dkt Godwin Maimu (Nnyaka).
“Nawaomba wasanii waamke na kujiunga na mfuko huu ili kwa pamoja tujikwamue kiuchumi”
Kwa upande wao balozi wa Tagoane, Mwanamuziki Shadrack Robert na wasanii wengine wasanii walisema wengi wao hukosa sifa ya kukopa kwa kushindwa kupata dhamana.
“Kwa hiyo Tagoane itatusaidia kusema kweli,” alisema mmoja wa wasanii hao, Shadrack Robert.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More