Saturday, April 28, 2018

TALGWU WAWATAKA WANACHAMA WAKE KUJIANDAA KUNUNUA HISA HAPO BAADAE ZA MICROFINANCE PLS


Baadhi ya viongozi wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa hapa nchini Tanzania (TALGWU)  wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda loa katika viwanja vya kichangani manispaa ya Iringa na kuwataka wanachama kununua hisa kwa wingiili nao wawe wamiliki wa taasisi na kufanikiwa kuwa na maamuzi ya chama hicho kwa maendeleo ya mwanachama 
Baadhi ya wananchi na viongozi walipokuwa wakibadilishana mawazo kwenye banda la TALGWU
 Baadhi ya viongozi wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa hapa nchini Tanzania (TALGWU)  wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda loa katika viwanja vya kichangani manispaa ya Iringa.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wanachama wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa hapa nchini Tanzania (TALGWU) wametakiwa kujiandaa kununua hisa hapo baadae za TALGWU microfinance PLC ili nao wawe wamiliki wa taasisi na kufanikiwa kuwa na maamuzi ya chama hicho kwa maendeleo ya mwanachama.

Akizungumza hii leo kwenye banda TALGWU katika maonyesho ya kuelekea mei mosi,mkurugenzi mtendaji wa microfinance PLC Jackson Ngalama alisema kuwa mwananchama wa TALGWUakinunua hisa atakuwa atapata gawio la kila mwaka kutoka na faida ambayo itakuwa imetengenezwa kwa kipindi hicho kutoka katika kampuni ya TALGWU microfinance PLC.


Ngalama alisema kuwa wananchama aliye na hisi katika kampuni ya TALGWU microfinance PLC ataruhusiwa kukopa kwa riba nafuu ambayo itamuongezea kufanya maendeleo binafsi tofauti naakienda kukopa sehemu nyingine.

“Sisi tunamlinda na kumheshimu mwanachama wetu hivyo hata akikopa atapewa elimu ya jinsi ya kutumia mkopo wake kwa faida maana tumeona watu wengi wakikopa huwa inakuwa vigumu kujua amekopa kwa ajili ya nini hivyo tumeamua kuta elimu kwanza ili kumfanya awe mwanachama mwenye mafanikio makubwa” alisema Ngalama

Ngalama alisema kwa sasa hisa zinatarajiwa kuuzwa kwa shilingi elfumoja na mwananchama anatakiwa kuanza kununua hisa za shilingi elfu hamsini na kuendelea ili kuongeza thamani ya kampuni hiyo na mteja wake anayetumtumia na kupata huduma hiyo.

“hisa zetu zinatarajiwa kuanza kuuzwa hivyo naomba nitoe rai kwa wanachama wetu wote waanze kujiandaa kununua hisa ambazo zitauzwa kwa gharama nafuu ya shilingi elfu moja tu.

Wakati huo huo afisa habari wa TALGWU Shani Kibwasali alisema kuwa TALGWU imekuwa ikiboresha na kuendeleza hali nzuri za wanachama wakiwa kazini,kuondoa tofauti zinazojitokezakati ya mwajiri na mwajiriwa  wakiwa kazini na kuwarudisha kuwa wamoja na kuendelea kufanya kazi na kuleta maendeleo.

“Sisi kazi yetu kuhakikisha mwanachama wetu anapata haki zakezote za msingi hivyo tunaposikia kunamgogoro mahali inatupaswa kwenda kuutatua na kuhakikisha kila mtu anapata haki yake” alisema Kibwasali

Kibwasali alisema kuwa TALGWU imefanikiwa kuishawishi serikali kuwarudisha wafanyakazi waliokuwa wamefukuzwa kazi mwaka 2017 kwa kuwa walikuwa wanaelimu ya kidato cha nne,mwaka 2016 hadi 2017 walishinda jumla ya kesi 37 zilizokuwa zinawakabili wanachama wakena pia walisimamia kutolewa kwa muundo mpya wa mwaka 2013/2014 wa watendaji wa kata,mitaa na vijiji.

Aidha Kibwasali alisema kuwa TALGWU imeweka mikakati ya mwaka 2016 hadi 2021 kwa kuhakikisha inawaunganisha wanachama wote kuwa kitu kimoja,kujenga na kuhimiza wanachama kuwa wawajibikaji wakiwa makazini,kuimalisha chama kiuchumi ili kutoa huduma inastahili kwa wanachama,kufanya ziara ya mara kwa mara ili kujua kero na changamoto mbalimbali zinawazowakabili wanachama wake

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More