Friday, April 6, 2018

MWENYEKITI WA CCM IRINGA ALBERT CHALAMILA ATOA ONYO KALI KWA WATAKAO TUMIA VIBAYA FEDHA ZA MNEC SALIM ASAS

 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Albert Chalamila akitema cheche kwa uongozi wa UWT mkoa wa Iringa

Na Fredy Mgunda,Iringa

CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimeagiza jumuiya umoja wa wanawake wa chama hicho (UWT) kusimamia vyema fedha walizopewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas kwa ajili ya kuimarisha miradi yao ya maendeleo yaliyokusudiwa na sio kuzitafuna kama njugu na  kwa malengo yao binafsi.

Agizo hilo limetolewa na mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Iringa Albart chalamila wakati akizungumza na umoja wa wanawake wa chama hicho na kuongeza kuwa wanataka    jumuiya hiyo iwe imara hivyo inatakiwa kuwa na uchumi imara ambayo itawawezesha kutimiza majukumu yanayotakiwa kama ambavyo wamepanga kufanya shughuli za kukuza uchumi.

Pia Chalamila alitoa angalizo kwa kiongozi yoyote wa umoja huo ambaye atatafuna fedha za miradi ya maendeleo au kukwamisha maendeleo atawajibishwa kwa mujibu wa sheria za chama ikiwa ni kufukuzwa uwanachama pamoja na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

 Alisema kuwa CCM ya sasa sio ya kuishi kimazoea kama iliyokuwa miaka iliyopita hivyo kila fedha itakayotolewa kwa ajili ya maendeleo ya chama itafuatiliwa hadi senti ya mwisho.

Niwaeleze ukweli CCM ya sasa sio kama ya miaka iliyopita miaka ya nyuma fedha nyingi zilikuwa zikitumiwa ndivyo sivyo sasa nikiwa kama mwenyekiti wa CCM mkoa nitahakikisha kufuatiliya hadi senti ya mwisho kwa lengo la kuhakikisha fedha zilizotolewa zinatumiwa kwa amalengo yaliyokusudiwa.” 
  
Aidha Chalamila alisema ili jumuiya hii iwe imara inatakiwa kuwa na uchumi imara ambayo itawawezesha kutimiza majukumu yanayotakiwa kama ambavyo wamepanga kufanya shughuli za kukuza uchumi.

Lakini Chalamila alisema MNEC Salim Asas amekuwa mdau mkubwa kwa kuchangia maendeleo ya chama cha mapinduzi na serikali kwa ujumla kwa lengo la kuboresha maendeleo na kuokoa maisha ya watanzania wengi wenye kipato cha chini.

“Amesaidia sana kuboresha sekta ya afya ,sekta ya elimu,sekta ya utalii na sekta ya miundumbinu hapa mkoani Iringa na kusaidia kuokoa maisha ya wananchi na kuongeza ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Iringa kwa ujumla” alisema Chalamila

MNEC salimu Asas anafanya kazi kubwa sana na hapaswi kubezwa hata kidogo kwa kazi zake za kuchangia maendeleo kwa wananchi wa kawaida hata wanachama wa chama cha mapinduzi ,hivyo ni muhimu kuhakikisha tunampa ushirikiano wa kutosha ili aendelee kuchapa kazi

 Awali akizungumza mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya Chama hicho MNEC Salim Asas alikabidhi kiasi cha zaidi ya Millioni 40 kwa umoja huo kwa lengo la kuimarisha miradi ya chama.

 Mnec alisema kuwa amekabidhi fedha hizo ambazo zitatumika kwa ajili ya kuanzisha miradi mipya na kukuza uchumi na kuacha kuwa omba omba.
“Zimetolewa fedha nyingisana hapa kwa ajili ya kukuza uchumi wa jumuiya hii kwa mkoa mzima hivyo mnatakiwa kuzitumia kwa malengo na sio kuzitafuta kama njugu.” alisema Asas

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo alitoa angalizo kwa umoja huo wasitumie fedha hizo kuanzisha migogoro kwenye jumuiya yao.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunaijenga CCM mpya ambayo itawaletea maendeleo wananchi wa mkoa wetu kwa sababu leo hii mnec ametusaidia na amekuwa mdau mkubwa sana,amechangia sekta mbalimbali ikiwamo afya,maji,elimu kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wanaoishi ndani ya mkoa wetu.”alisema Chalamila

Akizungumza mwenyekiti wa (UWT) mkoa huo Nikolina Lulandala licha ya kushukuru kupokea fedha hizo alisema atasimamia kuhakikisha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na hakuna hata senti itakayoptea kwa sababu wanataka kuwaletea wananchi maendeleo.

Lulandala alisema kuwa wanataka kuleta maendeleo kwa wananchi waliwaamini na kuwapa kura hivyo hawana budi kutorudisha fadhili lakini kubwa kuliko yote ni kuhakikisha 2020 wanakomboa jimbo la Iringa mjini ambalo linamilikiwa na mbunge wa jimbo hilo Mch.Peter Msigwa.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More