Thursday, April 12, 2018

MWENYEKITI WA BAVICHA MANISPAA YA IRINGA AIPONGEZA FAMILIA YA ASAS KWA KUBORESHA SEKTA YA AFYA


Wahenga wanasema hujafa hujaumbika. Na ule msemo usemao  kwamba  maendeleo hayana  vyama  ni hakika na bayana. 

Mwezi January mwaka huu nilikamatwa na jeshi la polisi na kuwekwa mahabusu kwa siku 8 kesi ya kisiasa , Hali hiyo ilimpelekea mke wangu Stellah ambaye alikuwa mjamzito kupata mshutuko na kuharibu mwenendo wa mimba yake. 

Jana usiku mke wangu ninayempenda sana hakuweza kuendelea kumlea mtoto akiwa  tumboni badala yake madakatari walihangaika kuokoa uhai wa mwanangu na mama yake na kazi hiyo walifanikisha kwa 100%.

Lengo la ujumbe huu ni shukrani za dhati kwa ASAS FAMILY waliojenga  jengo la kuokoa maisha ya watoto wachanga ASAS NEONATAL UNIT watoto ambao walikuwa wanapoteza maisha yao kila siku kutokana na vifaa tiba duni pamoja na ukosefu wa  wodi yenyewe ya kutunza ninaoweza kuwaita "Malaika wa Mungu".

Amenidokeza Nesi mmoja katika hosipitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa kuwa kwa juma moja kabla ya ASAS FAMILY kujenga jengo hilo kupitia Mkurugenzi wao SALIM  ABRI ASAS wameweza kupunguza kiwango cha vifo kutoka 20 mpaka vifo vya wachanga 2.

Nesi huyo ameendelea mbele na kunieleza kuwa ASAS haohao wamejenga Intesive Care Unit (ICU) ya kisasa ambayo imegharimu zaidi ya 300,000,000/= yenye uwezo wa kuhudumia mahutihuti 10 kwa mara moja ambayo bado haijazindiliwa. 

Ninajua wana Iringa wengi watapata huduma hapo kama mwanangu mwenye 850gm anavyopata huduma leo. 

I humbly acknowledge and pray for the blessings to the efforts made by this family to save hundreds of patients. 

Leonce Marto , 
Mkt BAVICHA IringaMjini.
12042018 .

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More