Monday, April 9, 2018

MBUNGE CHUMI AITAKA SERIKALI KUSAMBAZA MBOLEA KWA WAKATIMbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi ameitaka Serikali kuhakikisha inasambaza mbolea kwa bei nafuu na kwa wakati.

Chumi amesema hayo wakati akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu Bungeni.

'Mhe Mwenyekiti, serikali imekiri kuwa usambazaji wa mbolea ulikuwa 64% mana yake ni kuwa 36% ya wakulima hawakupata mbolea'

'Sio hivyo tu, hata hiyo 64% hawakupata mbolea kwa wakati, sio haki kabisa, mkulima wa Itimbo, Kitelewasi, Isalavanu apelekewe mbolea ya kupandia mwezi February wakati uandalizi wa mashamba unaanza mapema Oktoba.'

Kuzuia kuuza ziada ya mazao ni kuwaonea wakulima

Akizungumzia wakulima kuuza mazao yao,nje ya nchi, Chumi alisema kuna ziada ya tani 2.6milioni ya chakula, lakini Hifadhi ya Taifa ya Chakula imenunua tani 26,000(elfu ishirini na sita tu), afu mkulima anazuiwa kuuza mahindi yake, jambo ambalo sio sawa.

Tunawafanya wakulima wa nchi hii kama raia daraja la pili (second citizens),

mbolea tuwacheleweshee, ziada ya mazao yao tuwafungie kuuza, hii sio sawa' alisisitiza Mbunge huyo na kuongeza kuwa ni vizuri serikali ikaangalia changamoto ilizokutana nazo  katika usambazaji wa mbolea mwaka huu na kuboresha mazingira ili kumsaidia mkulima kupata mbolea kwa bei nafuu, kwa wakati na pia kuuza ziada ya mazao.

Awataka Wawekezaji Mafinga kuwajali wafanyakazi

Akizungumzia haki za wafanyakazi, Chumi alisema kuwa anapongeza jitihada za Rais John Magufuli kuvutia wawekezaji, lakini akaitaka Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Ajira kutupia jicho haki za wafanyakazi kwenye Viwanda vya Mafinga.

Uchumi wa Viwanda lazima uendane na welfare ya wafanyakazi, itakuwa haina mana kuwa na viwanda lakini hali za wafanyakazi zinakuwa duni, lazima walipwe vizuri, waangaliwe huduma za afya na kulipiwa nssf , alisisitiza Mbunge huyo.

Akifafanua, alisema sio haki mfanyakazi anatoka Changarawe, anatembea mpaka kilometa nne kwenda kazini, sio haki.

ni hatari sana, unakuta mama anaamka saa kumi alfajiri kuwai kazini ambako nako halipwi vizuri, nikuombe mama Jenista Mhagama (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu) na kaka yangu Mavunde (Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Vijana) nadhani ni mdogo wangu kufika Mafinga na kutoa maelekezo.

Apongeza Mhe Rais kukutana na Wafanyabiashara, ashauri akutane nao Kisekta

Tumeona ambavyo Jumuiya ya  wafanyabiashara walieleza kero zao na Mhe. Rais na Rais akaagiza Mawaziri wazifanyie kazi, lakini nimuombe Mhe Rais akutane na Wafanyabiashara kisekta mana siku ile wote tuliona muda ulikuwa mdogo kwa mfano anaweza kukutana na sekta ya usafirishaji.

Akizungumza baadae na Mwandishi wetu, Chumi alisema kuwa mazingira wanayofanyia kazi wafanyakazi kwenye Viwanda vya Mafinga hayaridhishi na wanapolalamika kwa baadhi ya viongozi taarifa hurejeshwa kwa wenye viwanda kwa siri na matokeo yake mlalamikaji hutafutiwa visa na kufukuzwa kazi.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More