Tuesday, October 31, 2017

MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE SERIKALI LIPENI MADENI YA WALIMU KWANZA

 Mwenyekiti chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi Obi Kimbale akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Baadhi ya walimu waliohudhuria mkutano mkuu wa chama hicho wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Na Fredy Mgunda,Mufindi

Chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimeitaka serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kutatua changamoto za walimu ili kukuza na kuboresha sekta ya elimu ambayo ndio kiungo muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote duniani.

Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho mwenyekiti wilaya ya Mufindi Obi Kimbale aliitaka serkali kulipa madeni wanayoidaiwa na walimu ili kuboresha maisha ya walimu ambao wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu.

“Walimu tunadai madeni ya malimbikikizi ya mishahara,madaraja tatizo kubwa na walimu wanadai madeni ya likizo hivyo walimu wanakuwa hawana morali ya kufndisha kutokana na kutolipwa stahiki zao kwa wakati” alisema Kimbale

Kimbale alisema kuwa kutoka mwaka 2016 hadi hii leo walimu wa wilaya ya Mufindi hawajalipwa stahiki zao hivyo kupunguza kasi ya walimu kuwa na wabunifu wakati kuandaa maandalio ya kwenda kuwafundisha wanafunzi ili  wapate elimu bora.

“Serikali ililipa madeni kidogo sana miaka ya nyuma hivyo bado serikali tunaidai pesa nyingi za walimu wa wilaya ya mufindi hivyo naitaka serikali kulipa madeni yote wanayodaiwa na walimu ili kuwaacha walimu wafundishe wakiwa huru kwa kupata stahiki zao zote” alisema Kimbale

Aidha Kimbale aliwaomba walimu kuendelea kuwafundisha wanafunzi kwa moyo wao wote wakati viongozi wao wanavyoshugulikia swala la madeni wanayoidai serikali.

Akijibu hoja hizo mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William alikiri kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu katika wilaya hiyo na kuahidi kuanza kuzitafutia ufumbuzi.

“Kweli kuna changamoto za miundombinu,stahikiza walimu na tatizo la upungufu wa walimu serikali inayafanyia kazi hayo yote ili kumfanya mwalimu afanye kazi yake kwa weledi unaotakiwa” alisema William

William aliwataka walimu kudhibiti nidhamu ya walimu na wanafunzi ili kumaliza tatizo utoro mashuleni ambao umekuwa ukisababisha wanafunzi wengi kushindwa kufaulu masoma yao na wengine kupata mimba wakiwa na umri mdogo.

“Mufindi kumekuwa na tatizo la wanafunzi wengi kupata mimba wakiwa na umri mdogo kutokana na utoro hivyo nawataka walimu kudhibiti nidhamu mashuleni na kupunguza hizi mimba za utotoni” alisema William
Aidha William aliwataka walimu kuacha kufanya siasa mashuleni ili kuboresha elimu kwa kizazi wanachokifundisha na kupata matunda mema hapo baadae.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More