Wednesday, October 25, 2017

WALIMU MANISPAA YA IRINGA WAMPIGIA MAGOTI MKURUNGEZI JUU YA VIWANJA

Katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa manispaa mwl. Fortunata Njalale akizungumza neno wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho manispaa ya Iringa uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa. 
Mwenyekiti wa chama hicho manispaa ya Iringa MWL. Zawadi Mgongolwa akizungumza neno wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho manispaa ya Iringa uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa akiwa sambamba na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka.  
Baadhi ya walimu waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa


Na Fredy Mgunda,Iringa

Chama cha walimu wa Tanzania (CWT) halmashauri ya manispaa ya Iringa kimemuomba mkurugenzi kuwakopesha viwanja walimu ili kujikwamuamua na mazingira magumu wanayokumbana katika nyumba wanazoishi.

Akisoma risala ya katika mkutano mkuu wa chama hicho manispaa ya Iringa katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alisema kuwa walimu wamekuwa wakiishi katika nyumba chakavu au mbali na mazingira ya shule kitu kinachosababisha kushuka kwa uwezo wa walimu kufundisha.

“Unamkuta mwalimu anakaa kihesa kilolo lakini anafundisha shule ya Tagamenda sasa ukiangalia umbali ni mrefu sana hiyo yote kutokana na kutokuwa na makazi katika eneo husika hivyo tunaomba kukopeshwa viwanjwa ili na sisi walimu tumiliki nyumba zetu” alisema Njalale

Njalale alisema kuwa walimu hawana pesa za kununua moja kwa moja viwanja hivyo kwa njia ya kuwakopesha inawezekana kutokana kuwa ni waajiliwa wa serikali na mishahara yao inajulikana na ni rahisi kuresha mkopo huo.

“Sisi walimu ukitaka kujua mimi nalipwa shilingi ngapi ni rahisi tu kwa kuwa mishahara ya serikali mara nyingi inajulikana hasa pale mtumishi unapoenda kukopa mahali ndio maana tunaiomba serikali itusaidie kukopa viwanja kuwa kuwa tunauwezo wa kulipa kwa awamu tatu” alisema Njalale

Aidha Njalale alimwambia mgeni rasmi kuwa ombi la walimu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa ni la muda mrefu hivyo wanamuomba alishughulikie ili walimu waweze kupata viwanja hivyo kwa nao wajenge nyumba zao.

“Njalale alisema kuwa walimu wanalipwa mishahara midogo lakini wanapanga nyumba kwa gharama kubwa kutokana na mazingira ya mjini yalivyo na bila kumsaidia walimu kutasababisha kutengeneza taifa lisilokuwa na wasomi wenye tija ya kuleta maendeleo” alisema Njalale

Akijibu risala hiyo katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka aliwataka uongozi wa walimu kuandika barua ya kuomba viwanja ili waweze kulishughulikia swala hilo likiwa kwenye maandishi.

“Andikeni barua yenye idadi na majina ya walimu wanaotaka viwanja ili kuondoa kasumba ya kusema wanaotaka ni kikukindi cha walimu wachache tu na bila kufanya hivyo swala lenu la kuomba viwanja litakuwa gumu kulitafutia ufumbuzi” alisema Chintinka

Chintinka aliwaomba walimu wawewavumilivu katika kipindi wacholishughulikia swala hilo kwa kuwa sio jambo la kukurupuka linahitaji utulivu wa kutosha ili kufanikishwa swala walimu kupata viwanja.



0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More