Thursday, October 26, 2017

MAAFISA ELIMU MANISPAA YA IRINGA KUKIONA CHA MTEMA KUNI KWA KUWANYIMA RUHUSA WALIMU

Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa  MWL. Zawadi Mgongolwa akizungumza wakati wa mkutono mkuu wa chama hicho manispaa ya Iringa katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa
Meza kuu wakiimba wimbo wa walimu wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wliaya ya Iringa manispaa
baadhi ya walimu waliohudhuria mkutano mkuu wa chama hicho

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa wameulalamikia utaratibu wa maafisa elimu kuwanyima ruhusa walimu kwenye matukio muhimu ya kitaifa na kwenye shida binafsi ambapo husababisha kushuka kwa morali ya kufundisha wanafunzi.

Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho mwenyekiti wa manispaa ya Iringa MWL. Zawadi Mgongolwa aliwatupia lawama maafisa elimu na walimu wakuu wa shule kwa kuwanyima ruhusa bila kuwa na sababu maalum.

“Mkurugenzi amekuwa ametoa kibali upewe ruhusa lakini viongozi waliochini ya mkurugenzi wanatuwekea vipingamizi ambavyo havieleweki kitu kinachozua utata mkubwa baina ya viongozi na walimu ambao sio viongozi” alisema Mgongolwa

Mgongolwa alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa kwa kuwajali walimu kwa kuwapa ruhusa pale inapotakiwa tofauti na hali ilivyo kwa hawa viongozi wa chini yake.

“Unakuta siku ya wanawake duniani au siku ya walimu duniani bado walimu wananyimwa ruhusa wakati muda huo mkurugenzi amewaruhusu walimu kuhudhuria sherehe hizo kitu kinachoongeza ukakasi baina ya watendaji wa nafasi za juu na watendaji wa nafasi za chini” alisema Mgongolwa

Aidha Mgongolwa alisema kuwa viongozi wa walimu wamekuwa wakipokea kero hiyo ambayo imedumu kwa muda mrefu kwa kushindwa kutafutiwa ufumbuzi hadi leo hii.

“Unajua mwalimu akikosa ruhusa huwa anajisikia vibaya na akitoka hapo sina uhakika kama mwalimu ataenda kufundisha vizuri kwa kuwa atakuwa tayari akiri yake ilikuwa kupata ruhusa ili aende akatatue matatizo yake” alisema Mgongolwa

Mgongolwa aliwapongeza walimu wa manispaa ya Iringa kwa kuendelea kufanya kazi kwa kujituma licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali ikiwepo kunyimwa ruhusa.

Akijibu hoja hiyo katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka alisema haelewi kwanini mara kwa mara swala hilo linakuwa linajirudia maana tulishalitafutia ufumbuzi hapo awali.

Sasa naenda kuandika barua rasmi kwa mkurugenzi ili kutatua kabisa tatizo hilo maana hata kwangu imekuwa kero na mwazoni nilijua wakuu wa shule ndio tatizo kumbe maafisa elimu ndio tatizo naenda kulishughulikia kwa haraka sana swala hili” alisema Chintinka

Chintinka aliwataka maafisa elimu na wakuu wa shule wote wa wilaya ya Iringa kuwapa ruhusa walimu pale ambapo wanapata matatizo maana hakuna haja ya kumnyima ruhusa mtu akiwa anashida na watakiwa kuzifahamu siku za kitaifa ambazo ni lazima walimu wahudhurie wanapaswa kutoa ruhusa bila kipingamizi.

“Kunasiku kama siku ya mwalimu,siku ya wanawake na siku nyingine za kitaifa walimu wanapaswa kupewa ruhusa kwenda kuhudhuria tukio hilo kutokana na umuhimu wake” alisema Chintinka

Chintinka alisema kuwa mkurugenzi ndio mwajili sasa hao maafisa elimu na wakuu wa shule wanatoa wapi hiyo jeuri ya kuwanyima ruhusa ambayo viongozi wa ngazi za juu wanajua kuwa kunakitu kinafanyika cha taifa.

Naye afisa elimu wa shule za msingi manispaa ya Iringa Samweli Mtovagakye alisema kuwa watawatafuta hao maafisa ambao wanawanyima ruhusa walimu wakati swala hilo lilishatafutiwa ufumbuzi.

“Jamani sisi huku sheria tulishaiweka kwenye matukio muhimu ya kitaifa walimu wapewe ruhusa sasa sijui ili sawala limetoka wapi naomba nikitoka hapa nitazungumza na wakuu wa shule pamoja na maafisa elimu wenzangu” alisema Mtovagakye


Mtovagakye aliwaomba walimu wampe muda ili aweze kulichunguza upya kwa nini swala hilo linajirudia mara kwa mara wakati walishalizungumza.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More