Tuesday, October 24, 2017

WAANDISHI WA HABARI WATANGAZA KUTOKUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI MKOANI GEITA

Mwenyekiti wa chama cha waandishi Mkoani Geita,Daniel Limbe Akisisitiza Msimamo wa waandishi wa habari wakati wa kikao cha waandishi wa habari Mkoani Geita.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa Habari Mkoani Humo wakati wa kikao cha maadhimio kwa Jeshi la Polisi.

Baadhi ya waandishi wa Habari Mkoani Geita wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya ofisi hizo.
 Na Joel Maduka.
 
Chama cha waandishi wa Habari Mkoani Geita Kimetangaza Kutokushiriki kazi zozote za Jeshi la Polisi kutokana na fujo ambazo wamekuwa wakifanyiwa waandishi wa habari wakati wakiwa kwenye majukumu yao ya kazi.




Uamuzi huo umefikiwa leo baada ya kumalizika kikao cha dharula cha waandishi wa habari ambao walikutana ili kujadiliana namna bora ya kukabiliana na unyanyasaji unaofanywa na jeshi la polisi kwa waandishi wa habari mkoani Geita.



Tamko la kuondoa ushirikiano kwa jeshi la polisi limesomwa na mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita Daniel Limbe (pichani),ambaye amesema uamuzi huo utatenguliwa iwapo uongozi wa Jeshi la polisi mkoani humo utajitokeza kuomba radhi kwa vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na polisi pamoja na kuwahakikishia usalama wao wawapo kazini.



Aidha uamuzi huo umeanza kutekelezwa baada ya tamko hilo huku ikielezwa kuwa mwandishi wa habari atakayekiuka makubaliano hayo atachukuliwa hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kufutwa uanachama wake ndani ya Klabu hiyo.





Uamuzi huo umekuja ikiwa ni siku mbili zimepita tangu waandishi wa habari wanne kushambuliwa na kuharibiwa vifaa vya kazi wakati wakichukua matukio ya vurugu zilizotokea kwenye shule ya sekondari Geita(Geseco) ambayo pia wanafunzi walikuwa wakitishia kuichoma moto iwapo wenzao watano waliokuwa wanashikiliwa na jeshi la polisi hawataachiliwa huru na kulejea shuleni hapo.





Waandishi waliokutana na masaibu hayo na vyombo vyao kwenye mabano ni Editor Edward(Mtanzania),Rehema Matowo(Mwananchi),Ester Sumira(Azam Tv) na Emmanuel Ibrahimu(Clouds tv).




0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More