Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limesema linatarajia kutoa
msimamo wao hivi karibuni kufuatia kauli ya Rais Magufuli ya kutoongeza
mshahara, mara baada ya vikao vyao na serikali kufanyika.
Katibu
Mkuu wa TUCTA, Yahya Msigwa amesema wanakusudia kuonana na uongozi wa
serikali ili kujadili suala hilo, na ndipo watatoa msimamo wao kama
hawatafikia makubaliano mazuri.
“Tunahitaji
kuonana na uongozi wa serikali tujadili, kuna mambo mengi ya kujadili
sio la mishahara tu, kwa muda mrefu vikao vimekuwa havikaliwi, hata
vikikaliwa havina majibu, sasa hivi lazima tulitafutie ufumbuzi kwa
sababu changamoto ni nyingi, wafanyakazi hawana hali nzuri kabisa,
malalamiko ni mengi mno”, amesema Yahya Msigwa.
Hapo
jana Rais Magufuli ametoa kauli ambayo imeibua sintofahamu nyingi kwa
wananchi, baada ya kusema hajaongeza mishahara na hatoongoze mishahara
kwa wafanyakazi kwa kipindi chote atakachokuwepo madarakani.
0 comments:
Post a Comment