- Itashutiwa katika miji ya Berlin, London, Paris, Cape Town na Acapulco, Mexico
Ø Mastaa wakubwa duniani kama Eric Dane wa Lastship ,Gerard Depardieu wa Life of Pie, Thomas Kretschmann wa Avengers Pearl Thusi wa Quantico…kushiriki
NYOTA
ya aliyekuwa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Mtanzania Idris
Sultan, inaendelea kung’ara baada ya
‘kupata shavu’ la kushiriki filamu yenye bajeti ya dola za Kimarekani milioni
17 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 38.
Idris
pamoja na Mtanzania mwingine Ernest Napoleon, wataungana na mastaa wakubwa duniani kama Eric Dame, mwigizaji Mmarekani, Gerard
Depardieu wa
Ufaransa, Thomas Kretschmann wa Ujerumani na wengine wengi kucheza filamu hiyo ya
ujambazi wa kimataifa.
Filamu
hiyo itakayojulikana kwa jina la ‘The Blue Mauritius’, inahusu majambazi watano
wa kimataifa ambao wanasafiri kwenda katika jiji la Cape Town nchini Afrika ya
Kusini, kwa ajili ya kuiba vitu mbali mbali vyenye thamani kubwa duniani.
Idris
na mwenzake Ernest Napoleon, watasafiri kwenda katika jiji la Cape Town nchini
Afrika kusini mapema mwakani kwa ajili ya filamu hii kubwa kuwahi kuwahusisha Watanzania.
“D
Street inayo furaha kubwa kugeukia vipaji vya waigizaji wa Kiafrika kwa
kuwaunganisha na waigizaji wa kimataifa kama itakavyokuwa kwa ‘The Blue
Mauritius’,” anasema Dexter Davis, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya D Street
Media Group ya Marekani, inayoanda filamu hiyo
Kwa
mujibu wa Davis, filamu hiyo itasambazwa siyo tu Marekani, bali pia katika
majumba makubwa ya sinema dunia nzima.
“Ernest
na Idris watang’ara, tunasubiri kwa hamu kuwaona tena kwenye skrini kubwa
wakifanya makubwa,” anasema Davis
Mapema mwaka huu, wawili
hao walicheza filamu iliyojulikana kama ‘Kiumeni’ ambayo pia Ernest alikuwa ni
mzalishaji na kushirikiana na Daniel Manege kuiandika. Filamu hiyo ilishinda
katika Tamasha la Timataifa la Filamu la Zanzibar ambalo Idris na washiriki
wenzake walihudhuria
“Ninayo furaha kubwa kufanya kazi na Idris
katika filamu kubwa kama hii ya The Blue Mauritius. Ni mwaka wa pekee kwa mimi
kufanikiwa kufanya kazi na D Street. D Street inabadilisha upepo kwa Afrika
inapokuja kwenye suala la kutengeneza filamu,” anasema Ernest
Kwa upande wake Idris
anasema, “Nilikutana Dexter Davis kwenye Maonyesho ya Filamu ya Kimataifa ya
Zanzibar mwezi Julai na nilifurahishwa na namna ambavyo amevutiwa na vipaji
kutoka Afrika. Alivutiwa kufanya kazi na mimi baada ya kuona ushiriki wangu
katika filamu ya ‘Ballin; On the Other side of the World’ na miezi miwili
baadaye nilishiriki Katina filamu moja ya Kimarekani. Filamu hizi mbili
zimenifanya niweze kufanya kazi nchini Marekani jambo ambalo nilitamani sana,”
Filamu hiyo inatarajia
kuanza kuzalishwa mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka ujao (2018).
MWISHO…………
0 comments:
Post a Comment