Mzoga wa kuku ambaye amefungwa na sanda kwa maelezo ya wananchi ambao walikuwa Nje ya Nyumba ya Bw Emmanuel Kabodi ambapo ndipo tukio hilo limetokea linalo husishwa na imani za kishirikina. |
Mama Mwenye Nyumba ambapo tukio hilo limetokea Bi,Scolastica Nicodemo akizungumza na moja kati ya viongozi wa dini wakati alipofika kwenye familia hiyo kuona tukio hilo la kusitajabisha. |
Baadhi ya wananchi wakishangaa jambo ambalo limetokea katika mtaa wa 14 kambarage. |
Viongozi wa dini wakiteketeza vitu pamoja na mzoga huo ambao umekutwa kwenye Nyumba hiyo. |
Baadhi ya watu wakishangaa tukio hilo la kusitajabisha. |
PICHA NA JOEL MADUKA
Katika hali
isiyo ya kawaida wananchi wa Mtaa wa 14 Kambarage Kata ya Buhalahala Wilaya na
Mkoa wa Geita wamejikuta wakipigwa na Butwaa
baada ya kukuta mzoga wa kuku ukiwa
umevishwa sanda kwenye familia ya
Emmanuel Kabodi.
Mama wa
familia hiyo Bi Scolastica Nicodemo ameelezea kuwa wakati
akifanya usafi aliona nyuma
ya geti kuna kitu kimefungwa na
shuka jeupe na alipojaribu kukiangalia aligundua ni sanda imefungwa kuku na ndipo walipofanya
maamuzi ya kumwita mchungaji kuja kujionea.
Askofu wa
kanisa la TMRC Mkoani Geita Stephano
Saguda ameihasa jamii kuachana na
maswala yanasosadikiwa kuwa ni ya
kishirikina kwani vitendo hivyo
havimpendezi Mungu na havikubaliki kwenye jamii ya watanzania .
Mjumbe wa
Mtaa Huo Stephano Mayovu Matata,amesema
tukio hilo ni mara ya pili kwani mara ya kwanza lilitokea tukio la
kufukuliwa kwa mtoto na kwamba ni vyema kwa mtu ambaye anafanya
vitendo hivyo kuachana navyo mara
moja kwani wakimbaini mtu wa namna hiyo
hawataweza kumvumilia.
Wananchi
ambao walikuwa wamekusanyika katika eneo hilo wamesikitishwa na kitendo hicho
kutokana na matukio hayo kuendelea kujitokeza mara kwa mara.
Mtaa wa 14 Kambarage umeendelea kukumbwa na
vitendo vinavyosadikiwa ni vya Imani za kishirikiana vya mara kwa mara na kusababisha
hofu kubwa kwa watu ambao wanaishi maeneo hayo.
0 comments:
Post a Comment