Tuesday, March 20, 2018

WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA AIPONGEZA MSD KATIKA MKUTANO WA 65 WA SADC

Image
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto), akimuonesha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  baadhi ya vifaa tiba vinavyosambazwa na Bohari ya Dawa (MSD), alipotembelea banda la MSD katika Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC). Kulia ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya. 
Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Mpoki Ulisubisya katika maonesho hayo.
Image

Maonyesho yakiendelea.


Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa zinazosambazwa na MSD.


Na Mwandishi Wetu



WAZIRI  Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameipongeza MSD kwa kuteuliwa kuwa mnunuzi mkuu wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC).

Waziri  Mkuu ametoa pongezi hizo alipotembelea  banda la MSD la maonyesho ambayo yanafanyika kando mwa  Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC).

Mkutano huo unajumuisha Mataifa tisa (9) wanachama ikiwemo Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More