Tuesday, March 6, 2018

MBUNGE RITTA KABATI AONGEZA MORALI KWA TIMU YA PANAMA GIRLS KUELEKEA MCHEZO WA KESHO DHIDI YA KIGOMA SISTERS

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati leo ametembelea kambi ya timu ya Panama Girls kwa kutoa amasa na zawadi kwa ajili ya kuwaongezea nguvu katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Kigoma Sisters ya mkoani Kigoma.
 Meneja wa uwanja wa ndege wa Nduli Anna Kibopile aliwapongeza timu hiyo kwa kuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu tofauti na timu nyingine za wanawake na kuahidi kununua kila goli kwa kiasi cha shilingi elfu kumi katika mchezo wa kesho. 
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwakabidhi msaada wa vyakula alivyowapelekea hii leo
 Baadhi ya wacheza wa timu ya Panama Girls ya mkoani Iringa walipokuwa wanamsikiliza mbunge Ritta Kabati na viongozi wengine walipotembelea kambini hii leo


 Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati leo ametembelea kambi ya timu ya Panama Girls kwa kutoa amasa na zawadi kwa ajili ya kuwaongezea nguvu katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Kigoma Sisters ya mkoani Kigoma.

Akizungumza katika kambi ya timu hiyo iliyopo eneo sabasaba Mbunge Kabati alisema kuwa anaipenda timu ya Panama kutokana na kuwa na wachezaji wa vipaji vya hali ya juu na ndio maana kila mwaka amekuwa akiichangia chochote alichonacho.

“Naomba kukiri kuwa mwaka huu sijaja kabisa nah ii ndio mara yangu ya kwanza kuja kuitembelea timu hivyo nahitaji kufunza vitu viti kutoka kwenu na kwa viongozi ili nikitoka hata nikavifanyie kazi kama nilivyofanya mwaka jana” alisema Kabati

Kabati akisema kuwa amewaletea vyakula kwa ajili ya kuongeza nguvu kwani mwanamichezo akila vizuri ndio atafanya vizuri hata uwanjani.

“Mnajua kuwa msipokula vizuri itakuwa ngumu sana kucheza uwanjani na mkapata ushindi hivyo nimeanza na kuletaa chakula hiki kasha nitazikuchukua changamoto zenu na kwenda kuzitafutia ufumbuzi” alisema Kabati

Aidha Kabati alisema kuwa atanunua kila goli litakalofungwa siku ya kesho kwa kiasi cha shilingi elfu ishirini na pesa hiyo itakuwa kwa matumizi ya wachezaji wote na kuwaomba kucheza kwa kujituma na kuhakikisha kesho wanapata ushindi wa kishindo ili kusahau machungu ya mechi ilipita.

Kwa upande wake meneja wa uwanja wa ndege wa Nduli Anna Kibopile aliwapongeza timu hiyo kwa kuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu tofauti na timu nyingine za wanawake na kuahidi kununua kila goli kwa kiasi cha shilingi elfu kumi katika mchezo wa kesho.

“Mimi nitanunua kila goli kwa shilingi elfu kumi hivyo naomba kesho fungeni magoli mengi ili pesa initoke nyingi kwa kuwa naipenda sana hii timu” alisema Kibopile

Naye makamu wenyekiti Mwanaheri Kalolo alimshukuru mbunge huyo kwa kujitolea mara kwa mara kuisaidia timu hiyo na kumuomba awatafutie wadau wengine wanaoweza kuisaidia timu hiyo kwa kuwa timu hiyo inauhitaji mkubwa wa pesa.



0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More