Thursday, March 15, 2018

WAKALA GYPSON CHAULA ASHINDA MILLION TATU KWENYE PROMOTION YA PUSH YA MTANDAO WA TIGO


 Meneja wa kanda za nyanda za juu kusini wa mtandao wa simu wa tigo Davis Kisamo akimkabdhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tatu wakala wa tigo pesa mkoani Iringa Gypson Chaula na makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za tigo mkoani Iringa 
Meneja wa kanda za nyanda za juu kusini wa mtandao wa simu wa tigo DavisKisamo akiwa na wafanyakazi wengine wa tigo pamoja na wakala wa tigo pesa mkoani Iringa Gypson Chaula wakiongea na waandishi wa habari katika ofisi za tigo mkoani Iringa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

WAKALA wa tigo pesa mkoani Iringa Gypson Chaula ameshinda kiasi cha shilingi million tatu (3,000,00)  katika promotion ya push inayoratibiwa na kampuni ya mtandao wa simu wa tigo nyanda za juu kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja wa kanda za juu kusini wa mtandao wa simu wa tigo Davis Kisamo alisema kuwa wamekuwa wakitoa zawadi mbalimbali kwa mawakala wa mtandao wa tigo wanaofanya vizuri kwa kuongeza miamala.

“Push promotion inasaidia kukuza mitaji ya mawakala wanaofanya vizuri kuwahudumia wateja wa kuweka pesa zao kwa mawakala,hivyo alifanikiwa kushinda ni yule wakala anayefanya miamala mingini kuliko wakala mwingine” alisema Kisamo

Kisamo alisema kuwa hii ni mara ya pili kwa mawakala kupata zawadi ya pesa kutoka mtandao wa tigo ili kuwafanya waipende kazi hii ya kuwa wakala na kuwa na uwezo wa kuwahudumia vizuri wateja wanapotaka huduma.

“Tunaangalia kuwa wakala kwa miezi mitatu anafanya nini na ameongeza kiasi gani cha wateja hivyo akifanya vizuri ni tunawapa zawadi hizi ili kuwaongezea nguvu kwa kutoa huduma bora kwa wateja wa mtandao wa tigo” alisema Kisamo

Aidha Kisamo Alisema kuwa promotion hiyo inawahusisha mawakala wote wa nyanda za juu kusini wanatoa huduma ya mtandao wa tigo na huwa wanapata zawadi mbalimbali kulinga na kufanya kwake vizuri kwa kuongeza miamala ya tigo pesa

Kisamo alimalizia kwa kuwaomba Tanzania kuendelea kutumia huduma inayotolewa na mtandao wa simu wa tigo kwa kuwa unatoa huduma bora ambazo zinasaidia katika maisha ya watanzania wengi.

Naye wakala wa tigo pesa mkoa wa Iringa Gypson Chaula aliishukuru kampuni ya mtandao wa tigo kwa kuwajali na kuwakumbuka mawakala kwa kuwapa motisha ambayo inachangia kuongezea mtaji.

“Mimi ninawapongeza sana viongozi wa mtandao wa tigo nyanda za juu kusini kwa kutujali na kuanzisha promotion hii ya push kwa kuwa inatuongea mtaji sisi mawakala” alisema Chaula

Chaula aliwataka watanzania kuendelea kutumia huduma za mtandao wa simu wa tigo kwa kuwa unatoa huduma nzuri kwa watumiaji wote wa mtandao huu.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More