Saturday, March 31, 2018

UWT IRINGA WATOA NEEMA KWA WATOTO YATIMA MKOANI HAPA

Katibu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Iringa Chiku Masanja akiwa mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iringa Ashura Jongo na katibu wa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati wakati walipowatembelea watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga nje kidogo ya manispaa ya Iringa kwa kuwafariji na kutoa msaada Katibu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Iringa Chiku Masanja akiwa mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iringa Ashura Jongo,katibu wa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati pamoja katibu wa umoja wa vijana mkoa wa Iringa (UVCCM) Mgego
Wadau mbalimbli pamoja na watoto yatima wakiwa wanasikiliza maneno ya kufariji kutoka kwa Katibu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Iringa Chiku Masanja 

Na Fredy Mgunda,Iringa.


Yatima wanaoishi katika kituo cha Tosamaganga mkoani Iringa wamepata neema kutoka kwa katibu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Iringa Chiku Masanja akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali ambao walifika kituoni hapo kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya sikuku ya pasaka kwa watoto hao.

Akiongea na waandishi wa habari kuhusu hatua hiyo ya kutoa msaada kwa watoto wanaokaa mazingira magumu, Masanja alisema kuwa lengo lao kubwa ni kujikwamua kwenye mazingira magumu na ikiwezekana kusiwepo kabisa na watoto tegemezi.

“Lengo letu kuu nikujikwamua kutoka kwenye mazingira magumu na kufuta kabisa uwepo wa watoto tegemezi kwenye jamii yetu” alisema Masenza

Aidha katibu Masanja alisema kuwa wanafanya hivyo kwa sababu watoto yatima wanaoishi kwenye mazingira yanayoonekana na yanayoizunguka jamii hivyo itapelekea wao kuondokana na upweke na kujisikia furaha kama watoto wengine wanaoishi mazingira ya kawaida.

Masanja alisema kuwa wameguswa kutoa msaada katika kituo hicho kwa kutenda matendo ya huruma wakati wa kipindi hiki cha sikuku ya Pasaka kwa watoto kwa kuwa wanamahitiji mengi pia ni kuwapunguzia ugumu wa maisha walezi wa watoto hao.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iringa Ashura Jongo alisema jamii inapaswa kuwajali yatima na wanyonge.

Jongo alisema watanzania ni jamii ya watu wanaopendana hivyo, watoto hao wanapaswa kuangaliwa kwa hali na mali ili wasihisi upweke wa kuwakosa wazazi wanapaswa kuangaliwa kwa jicho la tatu kwani hao ni wanyonge.

Lakini Jongo alisema inampasa kila mmoja kwa wakati wake kurudi mwenyewe na kuangalia namna ya kuwasaidia watoto hao wanyonge, kwani nao wanahitaji upendo na misaada mingine kama watoto wenye kulelewa na baba na mama

Nae Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Tosamaganga amewashukuru viongozi wote,wananchi wote pamoja na mkuu wa mkoa kwa kuwaona kwa jicho la pekee na kwenda kuwapa msaada katika kituo hicho.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More