Saturday, March 31, 2018

RC MASENZA ATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA TOSAMAGANGA

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masnza na viongozi mbalimbali wameanza kusherekea mapema ya Pasaka kwa kutoa msaada wa chakula na viu mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masnza na viongozi mbalimbali wakikabidhi mbuzi katika kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.

 Wadau mbalimbali waliojitokeza kutoa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.
Viongozi mbalimbali wa serikali waliojitokeza kutoa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.
 
Na Fredy Mgunda,Iringa.

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na viongozi mbalimbali wameanza kusherekea mapema ya Pasaka kwa kutoa msaada wa chakula na viu mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.

Watoto hao kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Kituo hicho, Sista Winfrida Mhongole, ni wale waliopoteza mama zao wakati wakizaliwa.

“Kituo kinapokea watoto wenye umri wa siku moja na kuendelea na tunaishi nao hapa kwa miaka saba kabla hatujawarudisha kwa ndugu zao waliowaleta,” alisema Sista Mhongole.

Pamoja na chakula hicho kilichojumuisha mchele, mbogamboga, mafuta ya kula na mbuzi, mkuu wa mkoa Masenza na viongozi wengine waliwapa watoto wanaoishi kituoni hapo zawadi zingine zilizojumuisha pipi na mafuta ya kupaka na kiasi cha zaidi ya shilingi lakini nne ambazo zilichangwa na wadau waliofika katika kituo hicho.

Masenza alisema kuwa ofisi yake inatambua umuhimu wa dhana ya maendeleo shirikishi na ndio maana wamekuwa wakijitolea kusaidia kuchangia shughuli zingine za kibinadamu mara kwa mara wanapopata fursa.

“Tulichotoa ni kidogo, lakini tunaamini kimesaidia kuwapa watoto hawa faraja na kujiona sawa na watoto wenzao waliopo majumbani kwao,”alisema.


Akishukuru kwa msaada huo, Sista Mhongole alisema mbali na watoto hao waliopo kituoni hapo, kituo kina watoto wengine katika shule mbalimbali za msingi, sekondari na vyuo ambazo kwa ujumla wake kinafanya kituo kiwe na jumla ya watoto 280.

Alisema watoto hao wamepokelewa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo ya Iringa, Mbeya, Njombe, Morogoro, Dar es Salaam na Morogoro.


“Mbali na mapato yatokanayo na shughuli za kilimo tunazozifanya kama kituo, kituo hiki kinaendeshwa kwa michango ya wahisani mbalimbali wa ndani na nje. Kwa kweli hatuna wafadhili wa kudumu,” alisema na kuomba wahisani waendelee kujitokeza kuwasaidia.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More