Mganga Mkuu wa Manispaa ya Iringa, May Alexander (kulia), akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Balozi Ali Mchumo (wa pilikushoto).Picha kutoka maktaba yangu.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Iringa umewataka wazazi na walezi kuwaingiza watoto wao katika mpango mpya wa huduma za matibabu kwa watoto chini ya umri wa miaka 918) unajulikana kwa jina la “Toto Afya Kadi” kwa lengo la kuwawezesha watoto kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wote.
Akizungumza na Mtanzania meneja wa bima ya afya mkoa wa Iringa dk Mohamed Kilolile alisema kuwa katika jitihada za kufikia lengo la afya bora kwa watu wote ,Mfuko wa bima ya afya (NHIF)umetanua wigo wake na sasa unasajili watoto katika huduma zake ili nao wapate huduma zao pindi wanapokubwa na matatizo ya ugonjwa.
Alisema kuwa mara nyingi wazazi wamekuwa wakitumia garama kubwa katika kuwahudumia watoto wao katika swala la afya na wakati mwingine kukosa fedha kwa ajili ya kuwatibu watoto wao jambo linoloweza wakati mwingine kusababisha kupoteza maisha lakini kwa kupitia huduma ya
toto afya kadi mtoto atatibiwa kwa mwaka mzima kwa shilingi 50,400/= sehemu yoyote atakayopenda mwanachama .
Kiholile alisema kuwa hii ni fursaa nyingine ambayo imetolewa kwa wazazi na walezi ambao ni wanachama wa mfuko lakini watoto wao hawakusajiliwa kutokana na ufinyu wa nafasi za utegemezi kuwa ni chache kwani mara nyingine mwanachama ana watoto sita lakini nafasi zilizopo ni 4 hivyo wanapaswa kutumia fursa hiyo kusajili watoto wao.
Alisema kuwa hii ni fursa ya kipekee pia kwa Watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata Bima ya afya kupitia wafadhili na wahisani mbalimbali ambao wangependa kuwasaidia ili pindi wanapopata matatizo
wawe na sehemu ya kupata Matibabu katika vituo Zaidi ya 600 nchi nzima
Kiholile alisema kuwa walengwa katika huduma hii ni watoto kuanzia umri wa mika (18) kushuka chini kutoka katika makundi mbalimbali kama watoto wote wa shule za awali, msingi na sekondari, Watoto wa kutoka vituo vya kulea watoto yatima na wasiojiweza ,Watoto waishio na wazazi/walezi bila kujali uhusiano walionao na kama wanasoma shule, au hawasomi
Hata hivyo aliwataka wakazi wote wa mkoa wa Iringa kuchangamkia fursa hiyo ya kipeke waliyokuwa wakiisubiri kwa muda mrefu kwa kuwandikisha watoto wao ili wanufaike kwa pamoja na huduma hiyo .
0 comments:
Post a Comment