Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella, ameagiza kurudiwa upya kwa zoezi la
uhakiki la kuabaini watumishi hewa katika mkoa wa Mwanza, ikiwa ni
mpango wa kubaini wale wote wanao lipwa mishahara bila kufanya kazi,
zoezi hilo litafatia zoezi lililo fanyika awali ambapo mkoa huo
ulibainika kuwa na watumishi hewa wapatao 334.
Mongella
amesema pamoja na kumalizika kwa zoezi la awamu ya kwanza la kuhakikiwa
kwa watumishi hewa na kubainika watumishi wapatao 334 tumeamua kufanya
upya zoezi hilo ili kuwa na idadi kamili ya watumishi wanaolipwa fedha
za serikali bila kuzifanyia kazi.
Amesema
tayari taratibu zinachukuliwa ikiwa ni pamoja kuunda jopo la kuhakiki
kutoka ngazi ya mkoa kwenda kwenye halmashauri zote za mkoa huo kwa
ajili yakufanya uhakiki upya wakiwa na Payroll.
“Nimesha
muagiza Katibu Tawala wa Mkoa, kuwa, Wakurugenzi wote kufika kesho(
leo) saa 6.00 kamili mchana yaani tarehe 05.04.2016 (Pay roll) zote ziwe
zimewasilishwa mezani kwake, ili wataalam kutoka ngazi ya mkoa waweze
kwenda nazo wilayani kwa ajili yakufanya uhakiki upya” alisema Mongella na kuongeza:
”Tunataka
kwenda kufanya uhakiki wa mtu kwa mtu (physical), popote pale walipo
warudi wahakikiwe labda kama yupo masomoni nje ya nchi."
Ameagiza
wale wote walioko masomoni, likizo au safari warudi mara moja kwenye
vituo vyao vya kazi kwa ajili ya zoezi la uhakiki, huku akiwataka wote
watakao kwenda kwa ajili ya kuhakikiwa waende wakiwa na picha tatu za
passport size, ambapo taratibu zakuweka kumbukumbu sahihi zitafanyika
“Tunataka
zoezi hili lichukue muda wa siku saba tu na baada ya hapo tutatoa
ripoti kamili, tusishangae kuona idadi hiyo ikiongezeka au kupungua
kwani katika uhakiki huu naamini tutapata majibu sahihi " alisema Mongella.
Aidha
alisema hata kuwa na mzaha na yeyote atakayebainika kulea matatizo ya
watumishi hewa katika mkoa huo, hivyo lazima kila mmoja awajibike kwa
nafasi yake aliyo ajiriwa nayo.
Katika
hatua nyingine Mongella, amevitaka vyombo vya habari katika mkoa huo
kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake ya
ulinzi na usalama, kusimamia maendeleo na kujua ustawi wa watu wa Mwanza
“Mwandishi
wa habari hatofautiani na kachero wa Polisi, sasa tusaidiane kuongoza
huu mkoa kwakupeana taarifa, maana mkoa huu ni mkubwa, sio rahisi kwa
Mkuu wa mkoa kujua yote yanayoendelea hadi ngazi ya kijiji lakini
kwakuwa ninyi wenzangu mnao wigo huo basi tusaidiane ili watu katika
mkoa huu waweze kufanya kazi zao kwa amani na salama."Alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza.
Imetolewa na: Atley J. Kuni
AFISA HABARI NA UHUSIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA
04.April,2016
0 comments:
Post a Comment