Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela au
kulipa faini ya Sh4.5 milioni, mfanyabiashara Huifang Ma baada ya
kupatikana na hatia ya kuuza bidhaa na kushindwa kutoa risiti kwa
kutumia mashine ya kieletroniki.
Ma ambaye ni raia wa China na mkazi
wa Mtaa wa Narung’ombe eneo la Kariakoo, alihukumiwa kifungo hicho
baada ya kukiri mashtaka mawili yaliyokuwa yakimkabili likiwamo la
kushindwa kujisajili kulipa kodi ya ongezeko la thamani (Vat).
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwanadamizi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Said
Mkasiwa alisema kwa kuwa mshtakiwa alikiri mashtaka yanayomkabili,
anatakiwa kulipa faini au kwenda jela miaka mitatu. Hata hivyo, Ma
alilipa faini na kuachiwa huru.
Katika hati ya mashtaka, ilidaiwa
kuwa Machi 23, mwaka huu eneo la Karikaoo, mshtakiwa alishindwa kutoa
risiti za kieletroniki kwa mteja wake.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo
mshtakiwa ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya HM Textile Co Ltd iliyopo Mtaa
wa Agrey, Kariakoo, alishindwa kutumia mashine za EFDs kwa ajili ya
kutoa risiti kwa wateja walionunua bidhaa dukani kwake.
Kosa la pili, mshtakiwa alishindwa kujisajili kama mlipa kodi wakati akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
0 comments:
Post a Comment