Mwanafunzi wa kidato cha tatu, juzi alimkaanga
askari polisi anayedaiwa kumbaka kwa kuieleza Mahakama jinsi
alivyotendewa kitendo hicho katika kibanda cha ulinzi cha benki.
Akitoa
ushahidi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Misungwi, Ruth Mkisi,
shahidi huyo alidai siku ya tukio askari huyo, Raphael Sixstus (30),
alimuita alipokuwa akipita karibu na Benki ya CRDB Tawi la Misungwi,
alipoitikia wito ghafla alivutiwa ndani ya kibanda hicho na kumbaka.
“Wakati
akinitendea kitendo hicho, alikuwa akinitishia kisu huku akiniambia
nikipiga kelele ataniua, niliogopa nikaa kimya ingawa niliumia na
kutokwa damu nyingi sana,” alidai shahidi huyo.
Akiongozwa
na Mwendasha Mashtaka wa Polisi, Doreth Mgenyi, mwanafunzi huyo mwenye
umri wa miaka 16 alidai kabla ya kumbaka, mshtakiwa huyo alimvua nguo
zote za ndani.
Awali, Mwendesha mashtaka alipokuwa akimsomea
makosa mshtakiwa huyo alidai kuwa Novemba 20, mwaka jana, akiwa eneo la
lindo katika Benki ya CRBD Tawi la Misungwi, alimbaka mwanafunzi huyo
saa 1.00 usiku wakati akitoka mashine kusaga unga katika maeneo ya
Bomani.
Hakimu Mkisi aliahirisha kesi hiyo hadi leo
itakapoendelea kusikilizwa kwa upande wa mashtaka kuita mashahidi
wengine. Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana.
0 comments:
Post a Comment