Waziri
wa Habari,Utamaduni,sanaa na michezo nchini,Nape Nnauye ametaja mambo
manne ambayo ni vikwazo ndani ya sekta ya sanaa ya filamu nchini na
kuyaita kwamba ni majipu huku akisisistiza kwamba serikali itakwenda
kutunga sera ya sekta hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17.
Nape,aliyataja
mambo hayo na kuyafananisha na majipu kuwa ni uporaji wa kazi za
wasanii nchini,ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za wasanii
nchini,usimamizi mbovu wa bodi ya filamu nchini sanjari na tatizo la
mfumo mbovu wa usambazaji wa kazi za wasanii nchini.
Akizindua tamasha la filamu la Tanzanite International Film
Festival(TIFF)
jijini Arusha juzi ambao ulihudhuriwa na wasanii maarufu wa filamu
nchini waziri huyo alisema kwamba jipu la kwanza ambalo atakwenda
kulitumbua ni uporaji wa kazi za wasanii nchini.
“Jipu
la kwanza tutalitumbua kwenye bajeti yetu ya mwaka 2016/17 ni uporaji
wa kazi za wasanii nchini wengi wananyonywa jasho lao”alisema
Nape
Hatahivyo,alisema
kwamba jipu la pili ni ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za wasanii za
filamu nchini na kudai kwamba chini ya uongozi wake atahakikisha
anaimarisha miundombinu bora kwa lengo la kuwasaidia wasanii hao pamoja
na kulinda haki zao.
Alisema
ya kwamba mfumo wa kazi za usambazaji wa kazi za wasanii nchini pamoja
na hakimiliki ni wa kinyonyaji huku akitolea mfano wa kazi za msanii
maarufu wa sanaa hiyo nchini marehemu Stephen Kanumba na kusema kwamba
familia yake hainufaiki na matunda ya kazi zake hadi sasa kutokana na
mfumo mbovu wa usimamizi wa kazi za wasanii nchini.
Alitaja takwimu kwamba mwaka 2011/12 jumla ya filamu 218
zilitengenezwa
nchini na mwaka 2014/15 kazi hizo ziliongezeka hadi kufikia 14,00 huku
akidai hilo linadhihirisha kwamba sekta hiyo inakua kwa kasi nchini na
kuongeza ajira
Hatahivyo,Rais
wa shirikisho la wasanii wa filamu nchini(TAFF),Simon Mwakifamba
aliwataka wasanii wa filamu nchini kujiandaa kisaikolojia kukabiliana na
soko la ushindani wa filamu duniani kwa kuwa wabunifu.
“Serikali tunaiomba iandae sera itakayoandaa mazingira mazuri kwa wasanii nchini kuhusu usalama wa kazi zao”alisema Mwakifamba
Naye,
muaandaji wa tamasha hilo,Said Sassi alisema kwamba tatizo la uharamia
wa kazi za wasanii nchini limetanda na kuwaomba wafanyabiashara na
makampuni kujitokeza kudhamini vipindi mbalimbali vya luninga kwa lengo
la kuinua sekta hiyo.
Mkurugenzi
wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya vito ya Tanzanite One Mining Ltd
ambao ni miongoni mwa wafadhili wa tamasha hilo,Feisal Shabhai alisema
lengo la kampuni yao kujitosa kufadhili tamasha hilo ni kutoa mchango
wao katika kusaidia jamii kupitia faida wanayoipata ili kuinua sekta ya
ajira nchini.
0 comments:
Post a Comment