Wananchi
wamemkataa mwenyekiti wa kitongoji cha Mwanogi kijiji cha Bulima, Kata
ya Nyashimo wilayani Busega katika Mkoa wa Simiyu, wakimtuhumu kuweka
majina hewa katika mradi wa kuokoa kaya masikini unaosimamiwa na Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).
Mwenyekiti huyo wa kitongoji, Ester Ng’ombe anatuhumiwa pia kufanya kazi kwa ubaguzi wa vyama vya siasa.
Akizungumza
katika kikao, mwenyekiti wa kamati ya mipango na fedha ya kijiji cha
Bulima, Zablon Ntinika alisema wamefikia uamuzi wa kumsimamisha kazi
mwenyekiti huyo baada ya uchunguzi walioufanya kubaini majina matano
ambayo ni hewa yakipatiwa fedha.
Alisema
wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mwenendo wa mwenyekiti huyo katika
utendaji wake wa kazi katika kitongoji hicho lakini wamebaini mengi.
Mwenyekiti huyo anayetuhumiwa, alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema kuwa yeye hayatambui bali ni siasa za chuki dhidi yake.
Ng’ombe
alisema chanzo si majina feki bali ni siasa zinazochochewa na wanasiasa
wa kata hiyo ambao wanataka kuichafua sifa yake ili aweze kuondolewa na
wananchi waliomchagua.
0 comments:
Post a Comment