Wednesday, April 20, 2016

JUNAYSATY kuwasha moto siku ya Mkwawa Talent Search(MTS) linatarajiwa kufanyika april 30 mwaka huu mkoani Iringa




NA RAYMOND MINJA IRINGA

Lile Shindano la kusaka na kuibua  vipaji vya uimbaji lijulikanalo kama Mkwawa Talent Search(MTS) lenye washiriki zaidi  72 linatarajiwa kufanyika april 30 mwaka huu mkoani Iringa na kuhudhuriwa na wasani mbalimbali toka nyanda za juu kusini


Shindano hilo la kwanza kufanyika mkoani Iringa na litakalo  katika ukumbi wa luxary pab linatarajiwa kutikisa anga la nyanda za juu kusini kutokana na kujitokeza wasani wengi wenye uwezo mkubwa katika uimbaji

Akizungumza Na mtanzania mratibu wa mashindano hayo ambayo pia yanasimamiwa na Radio Cantry fm radio ya mjini  Kayanda Manyanya alisema kuwa wameamua kuanda mashindano hayo ili kuweza kuwasaidia
wasani wadogo kuweza kuonyesha vipaji vyao katika leval nyingine .

Manyanya alisema kuwa nyanda za juu kusini kuna vipaji vya aina mbalimbali ikiwemo uimbaji lakini wamekosa watu wa kuwainua  kimuziki hivyo kupitia shindano hilo wanamini wako wasani watafanikiwa na kuanza kujulikana kimataifa .


Alisema ili kuwapa motisha wasani hao mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajinyakulia shilingi laki 500.000,mshindi wa pili shilingi laki 300,000 na mshindi wa tatu akijinyakulia shilingi laki 200,000 pamoja na kurekodiwa audio  na video .

“Hiii ni fursa kwa vijana wetu kujituma na kufanya kazi nzuri ambayo itawashawishi majaji na mashabiki kuweza kumpigia kura na ili zimuwezeshe kushinda mana licha ya zawadi hizo pia watapata nafasi ya kufanyiwa promo ili kuweza kumfanya kujulikana Zaidi ”

upande wa washiriki wa shindano hilo kutokea kihodombi Junaysaty anayefanya mziki wa bongo fleva alisema kuwa kuja kwa mashindano hayo kutawasaidi wasani  kufanya vema kimuziki na kuachana na dhana ya wasani wachanga kuombwa ruswa ya ngono ili kutoka kimuziki
  .

Alisema kuwa swala la kipato limekuwa ni changamoto kubwa kwa wasani wadogo  katika kufanikisha kutengeneza kazi zao hali inayowalazimu baadhi ya wasani wa kike kujirahisisha kwa maproduza ili kuweza
kutengeneza kazi zao hali inayowadhalilisha katika jamii kuonekana wote wako .

“Binafsi mii inaniuma sana kuona mtu anatoa rushwa ya ngono ili afanikiwe kimuziki huu ni udhalilishaji wa hali ya juu  kama unakipaji wewe utatoka tu kimuzi sio lazima mpaka ufanye hivyo mbinafsi yangu na mshukuru mume wangu yuko bega kwa began na mimi katika kusaidi kazi
zangu za muziki hivyo sipati shida katika hilo  yeye na mwanangu ndio kila kitu kwangu nawapenda Sanaa”.

Hata hivyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali kuweza kujitokeza kwa wingi ili kuwasaidia wasani wadogo kuweza kufanya vizuri kazi zao huku akijinasibu kuibuka kidedea katika shindano hilo kwani anaamini kuwa
yeye anafanya vizuri katika game la muziki wa kizazi kipya kutokana na shangwe anazopata kutoka kwa mashabiki wake

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More