Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki amesema Halmashauri
Wilaya ya Rombo iko hatarini kufutwa kutokana na kushindwa kufikia lengo
la Serikali la kukusanya mapato kutoka kwenye vyanzo vyake.
Sadiki alisema hayo jana wakati akizungumza na madiwani, wenyeviti wa vijiji na wakuu wa idara wa halmashauri hiyo.
Alisema
wilaya hiyo inatumia asilimia 93 ya ruzuku kutoka serikalini hali
inayosababisha kuwa hatarini kufutwa kwa kushindwa kukusanya mapato.
Mkuu
wa wilaya hiyo, Lembris Kipuyo aliitaka halmashauri hiyo kubuni vyanzo
vipya vya ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo iliyojiwekea.
Alisema
Serikali imetangaza halmashauri ambazo zitashindwa kukusanya mapato na
kufikia asilimia 80 ifikapo Juni mwaka huu zitafutwa.
“Serikali haina
lelemama ikifika hiyo tarehe kama mmeshindwa kufikia lengo itafutwa,
taarifa nilizonazo mko asilimia 43 hali ambayo ni hatari kwa halmashauri
ambayo iko mipakani mwa nchi nyingine,” alisema Sadiki.
0 comments:
Post a Comment