Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa nchini (Nida) imesema itaanza kufanya malipo
ya madai ya wafanyakazi wake 597 waliokatishwa mkataba na mamlaka hiyo
hivi karibuni.
Taarifa
iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Modestus
Kipilimba, ilisema malipo hayo yataanza kulipwa kesho asubuhi kwenye
ofisi za mamlaka hiyo zilizopo katika jengo la BMTL.
Malipo
hayo yatafanywa kwa mgawanyo. Mgawanyo wa kwanza utakuwa na kundi la
kwanza, pili na tatu, ambao watalipwa kesho na mgawanyo wa pili, utakuwa
na kundi la nne na tano ambao watalipwa keshokutwa.
Mgawanyo
wa tatu utakuwa na kundi la sita litakalo lipwa Alhamisi, mgawanyo wa
nne utahusisha kundi la 7 na 8 litakalolipwa Aprilu 16 na kundi la tano
litajumuisha madereva na kada nyingine, litalipwa Aprili 17.
Aidha,
taarifa hiyo iliwataka wadai hao kufika kwa wakati sambamba na kuwa na
vielelezo na nakala halisi za mikataba yao ya kazi.
Awali,
kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wafanyakazi hao walioandamana baada
ya tangazo la kufutwa kazi kuwa malipo yanayotarajiwa kutolewa na Nida
hayasadifu uhalisia wa kile wanachokidai.
0 comments:
Post a Comment