Mfanyabiashara anayemiliki Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd, Said Lugumi, ametoroka nchi.
Lugumi
ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wa kupindukia katika kipindi kifupi,
aliingia mkataba tata na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa ajili ya
kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108
nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37.
Taarifa
za kutoroka nchi kwa mfanyabiashara huyo, zilielezwa na baadhi ya
maofisa wa vyombo vya dola, ambapo inadaiwa kuwa aliondoka nchini
Jumatatu wiki hii, siku ambayo Jeshi la Polisi lilitakiwa kuwasilisha
mkataba huo Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa mujibu wa
sheria.
Mfanyabiashara
huyo ambaye amekuwa akitembea na msafara mkubwa wa magari ya kifahari,
huku akilindwa na walinzi maalumu wa kukodi, ametoroka wakati vyombo vya
dola vilikuwa vikimuwinda.
Utata wa Malipo
Pamoja
na hali hiyo inaelezwa kuwa licha ya Lugumi kuingia mkataba na Jeshi la
Polisi wa Sh bilioni 37, lakini bado alilipwa Sh bilioni 46 nje ya
mkataba.
Katika
mkataba huo, alilipwa kiasi Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99
ya fedha za makubaliano ya mkataba, lakini hadi sasa mashine hizo
zimefungwa katika vituo 14 pekee jijini Dar es Salaam ambavyo hata hivyo
haijaainishwa maeneo vilipo.
Sakata
hili lilibainika wiki iliyopita baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), kukutana na maofisa wa jeshi hilo kupitia taarifa ya
hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu
wa Hesabu za Serikali (CAG).
Msafara wake Wapungua
Duru
za ndani zinaeleza kuwa tangu Kamati ya Bunge ilipoibua sakata hilo na
vyombo vya dola kuanza kuwahoji baadhi ya washirika wake katika
biashara, msafara wa mfanyabishara huyo umepungua.
Chanzo
kimoja kinasema kwa mara ya mwisho mfanyabiashara huyo alionekana eneo
la Oysterbay jirani na Kanisa la St. Peter, huku akiwa na magari mawili
badala ya saba hadi 10 kama ilivyokuwa awali.
Mtoa
habari huyo alisema Lugumi aliopoonekana mwishoni mwa juma lililopita,
alikuwa na magari mawili likiwamo Toyota GX V8 toleo la mwaka huu,
ambalo lilikuwa limebeba walinzi wake, huku mwenyewe akiwa ndani ya gari
la kifahari aina ya Escalade.
“Lugumi
anaishi Mbweni na awali ilikuwa msafara wake ukipita magari
husimamishwa ili kumpisha, na huwa na magari mengi kweli mithili ya
kiongozi wa nchi, jamani kuna watu wamejua kuitafuna nchi hii, na sasa
huenda unatimia usemi wa Rais Magufuli kuwa ni zamu yao kuishi kama
mashetani na si kama malaika,” kilisema chanzo hicho.
Mkataba Wahamishwa
Sakata
la mkataba huo wa Polisi na Lugumi limezidi kuchukua sura mpya baada ya
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kunyang’nywa hoja hiyo na
badala yake kuhamishiwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama.
Hatua
hiyo inatokana na utata uliogubika mkataba huo ambao unawahusisha
vigogo kadhaa wa Jeshi la Polisi pamoja na baadhi ya watendaji wa
Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, huku ikidaiwa kuwa huenda ikawa njia
ya ‘kulindwa’.
Kutokana
na hali hiyo, hadi kufikia Jumatatu saa 10 jioni, Makamu Mwenyekiti wa
PAC, Aeshi Hilaly, alisema kuwa kamati yao haijapokea taarifa yoyote
kuhusu Kampuni ya Lugumi, ambapo kamati hiyo ililitaka Jeshi la Polisi
kuwasilisha mkataba huo hadi kufikia leo.
Aeshi
alisema wamemuomba Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, ili aweze
kuwaandikia Polisi barua kwa ajili ya kuwasilisha mkataba huo.
“Tumelazimika
kumwandikia barua Katibu wa Bunge ili awaandikie barua polisi walete
mkabata huo ndani ya siku tatu kutoka leo (juzi) kama walivyotakiwa na
kamati yetu,” alisema Hilaly.
Kauli ya Bunge
Alipotafutwa
Mkuu wa Idara ya Habari, Elimu na Mawasiliano, Ofisi ya Bunge, Owen
Mwandumbya, alisema kama kuna hoja iliyoibuliwa na Kamati ya PAC kisha
ikapelekwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,
itakuwa ni kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusu matumizi ya fedha.
“Kama
suala hilo lipo Mambo ya Nje, itakuwa si kwa hoja iliyoibuliwa na PAC
na hakuna suala linaloshughulikiwa kama limeanzia PAC.
“Na
kama litakuwa limekwenda huko ni kwa ajili ya kupata uelewa kuhusu
matumizi ya fedha, na unajua hivi sasa hizi kamati zipo katika
maandalizi ya bajeti. Ila hoja kuhamishiwa kamati nyingine hutokana na
maelekezo ya Spika wa Bunge. Kwa hoja hii ya PAC bado suala hilo lipo
chini yao,” alisema Mwandumbya.
Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment