Mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani
ambaye amekuwa akiongoza kwenye kinyang’anyiro hicho, Donald Trump
amejikuta akikosolewa vikali kuhusu upeo wake juu ya sera za nje pale
aliposhindwa kulitamka bayana jina la Tanzania.
Drump ambaye
Jumanne aliyopita alivuna ushindi wa kishindo kwenye majimbo yote manne
yaliyopiga kura za mchujo alijikuta akitumbukia kwenye kadhia hiyo
wakati akielezea vipaumbele vya Marekani kuelekea mataifa ya kigeni.
Alikuwa
akigusia juu ya mashambulizi ya mabomu yaliyotokea katika ubalozi wa
Marekani nchini Tanzania na Kenya na kusababisha uharibifu mkubwa wa
mali huku watu kadhaa wakipoteza maisha.
Akiwa katika hali ya
kujiamini, Trump alisema kuwa iwapo ataingia madarakani moja ya
vipaumbele vyake ni kuendelea kutetea masilahi ya Marekani na
kudhihirisha hilo aliamua kutolea mfano mashambulizi hayo ya kigaidi.
Lakini
wakati akilitaja jina la Tanzania, mfanyabiashara huyo alijikuta
akigusa hisia za wengi pale alipolitaja jina hilo kinyume na
inavyotamkwa. “ Ona mashambulizi yaliyotokea katika miaka ya 1990 katika
ubalozi wetu nchini Tan-ZAY-nee-uh”.
Matamshi hayo yalizusha
mjadala mkubwa huku baadhi ya wakosoaji
wake wakiingia kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kumuelezea kama ni
mtu asiyekuwa na upeo mkubwa kuhusu siasa za kimataifa.
Baadae kambi ya kampeni ya Trump ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikisema kuwa kuteleza kwa mgombea wao katika matamshi ya jina halisi la Tanzania hakumaanishi kuwa uwezo wake kuhusu masuala ya usalama,diplomasia ya kimataifa na biashara ya kimataifa ni wa kutiliwa mashaka.
Baadae kambi ya kampeni ya Trump ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikisema kuwa kuteleza kwa mgombea wao katika matamshi ya jina halisi la Tanzania hakumaanishi kuwa uwezo wake kuhusu masuala ya usalama,diplomasia ya kimataifa na biashara ya kimataifa ni wa kutiliwa mashaka.
0 comments:
Post a Comment