Dokta
Abdull Maulid Abdull akimpima Miwani ya kuonea Mwananchi Chale Muumin
Fumu mkaazi wa Kijiji cha Matemwe Tunda ngaa katika matibabu yalio
fanyika skuli ya matemwe mkoa wa Kaskazini unguja.Dokta Rajab Mohd(picha kutoka maktaba)
NA RAYMOND MINJA IRINGA
MADAKTARI Bingwa wa Magonjwa sugu na magonjwa mbalimbali
wanatarajia kutua mkoani Iringa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa
ambao walishindwa kusafiri kutoka mikoani kufata huduma hizo katika hospitali kubwa .
Kuja kwa madaktari hao bigwa kunaelezwa kuwa kutawarahisishia wananchi kupata huduma
kwa garama ndogo tofauti na wagonjwa hao wangesafiri umbali mrefu kufuata
huduma hiyo .
Hayo yamesemwa Meneja wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Iringa
Dk. Mohamed Kilolile wakati akizungumza na Mtanzania ofisini kwake juzi kuhusu ujio wa
madaktari bingwa ikiwa ni lengo la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuwapeleka
madaktari bingwa katika mikoa ya pembezoni mwa nchi kwa ajili ya kutoa huduma
za uchunguzi wa kina na kutibu wanachama
wa Bima ya Afya pamoja na wagonjwa wengine wa kawaida.
Dk Kilolile alisema kuwa lengo la madaktari hao kutoa huduma
hiyo mkoani Iringa na mikoa ya jirani ni kuweza kuwarahisishia wananchi wa
kuweza kupima na kujua afya zao na kupunguza gharama kwa wale ambao hawana kadi
za bima ya afya ambapo zoezi hilo litafanyika pia mkoa wa Njombe.
Alisema kuwa huduma ya madaktari bingwa zitafanyika
katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kuanzia April 25 hadi 30 na
kuwataka wananchi mbalimbali kujitokeza kuweza kupata huduma ya matibabu kwa
wale wenye kadi za bima ya afya na wasio na kadi watatibiwa kwa gharama zinazotozwa hospitali hapo .
“ Mfuko wa bima ya afya kwa wajali watumishi na wateja wa bima ya afya
huwa unaandaa mipango ya kuboresha huduma zake hivyo mwaka huu madaktari bingwa
watakuwepo mkoani Iringa kwa lengo kila mtu aweze kujielewa afya yake kwani
endapo utapojua afya yako baada ya kufanya vipimo itakuwa rahisi kupata
matibabu ambayo tayari ushaletewa hapohapo karibu bila kuifuata sehemu za mbali
“Alisema
Alisema kuwa madaktari hao ni mabingwa katika wa maradhi
mbali mbali yakiwemo magonjwa ya nje na ndani ,kisukari, usingizi, kinywa na
meno magonjwa ya Moyo, huduma za mama na
mtoto na magojwa mengineyo.
Hata hivyo Kiholile aliwataka wazazina walezi kuwaingiza watoto wao katika
mpango mpya wa huduma za matibabu kwa watoto chini ya umri wa miaka (18)
unajulikana kwa jina la “Toto Afya Kadi”
kwa lengo la kuwawezesha watoto kuwa na uhakika wakupata matibabu wakati wote.
Kilolile alisema kuwa katika jitihada za kufikia lengo la afya bora kwa watu wote ,Mfuko wa bima ya afya (NHIF)umetanua wigo wake na sasa unasajili watoto katika huduma zake ili nao wapate huduma zao
pindi wanapokubwa na matatizo ya ugonjwa.
Alisema kuwa mara nyingi wazazi wamekuwa wakitumia garama kubwa katika kuwahudumia watoto wao katika swala la afya na wakati mwingine kukosa fedha kwa ajili ya kuwatibu watoto wao jambo linoloweza wakati mwingine kusababisha kupoteza maisha lakini kwa kupitia huduma ya
toto afya kadi mtoto atatibiwa kwa mwaka mzima kwa shilingi 50,400/= sehemu yoyote atakayopenda mwanachama

0 comments:
Post a Comment