SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limeingia kwenye orodha ya Taasisi za Serikali zenye matumizi makubwa ya fedha ukilinganisha na mapato wanayokusanya, jambo lililoishtua Kamati ya Bunge na kutaka shirika hilo lipunguze matumizi yake.
Hayo
yalibainika jana Dar es Salaam wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), ilipokutana na Tanapa kupitia ripoti
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka
2013/14.
Katika
ripoti hiyo ilibainika kwamba Tanapa kwa mwaka huo wa fedha, ilitumia
jumla ya zaidi ya Sh bilioni 151.7 ilhali mapato yao yalikuwa Sh bilioni
149.9 hivyo matumizi ya fedha yaliyozidi ni Sh bilioni 1.8.
Taasisi
nyingine ya Serikali ambayo ilikuwa na matumizi makubwa ya fedha za
Serikali ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ripoti ya CAG
ya mwaka 2013/14 ilionesha kuwa ilitumia Sh bilioni 18.6 kwa ajili ya
matumizi ya watumishi wake.
Wakichangia
hoja mbalimbali wakati wa kupitia ripoti hiyo hapo jana, Wajumbe wa
Kamati hiyo walisema kutokuwepo Bodi ya Shirika hilo, kunachangia
watendaji wa shirika hilo kuliendesha ndivyo sivyo.
Mjumbe wa Kamati hiyo, Albert Obama, mbunge wa Muhigwe alisema shirika hilo ni jipu
kwa sababu limejilimbikizia ulaji, kana kwamba ni chombo cha watu
wachache, ilhali shirika hilo linatakiwa liwe kwa ajili ya ustawi wa
uchumi wa nchi.
“Haiwezekani
ripoti ya mwaka 2013/14 inaonesha kuwa mapato yenu yalikuwa Sh bilioni
149.9 halafu matumizi yenu ni Sh bilioni 151.8”, yaani mnatumia chote
hadi mnadaiwa sasa hii sio sawa, hili ni shirika la umma?” Alihoji Obama.
“Hapa
wanakuja na maneno matamu kwamba bajeti ya mwaka huu 2016/17 wamepanga
kukusanya mapato ya Sh bilioni 188 lakini matumizi yenu pia mmeainisha
yatakuwa Sh bilioni 270, hii ikoje? " Alihoji Obama.
Mjumbe
mwingine, Joseph Kakunda mbunge wa Sikonge, alisema Tanapa haina
changamoto kubwa, zinazoifanya ishindwe kukusanya mapato makubwa zaidi
ya hayo ya sasa na kusema walipaswa kukusanya zaidi ya Sh trilioni moja
na sio hizo bilioni 149.
0 comments:
Post a Comment