IMEELEZWA
kwamba
idara ya afya katika mkoa wa Iringa ndiyo Sekta inayoongoza kwa
malalamiko ya kuomba na kuchukua rushwa.
Kauli
hiyo imetolewa na mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru)
Mkoa wa Iringa, Eunice Mmari wakati akizungumza na wanahabari mjini
hapa na kusema kuwa taasisi hiyo imepokea malalamiko 28 ya rushwa na 14
kati ya hayo yamefunguliwa majalada ya uchunguzi na malalamiko tisa bado yanafanyiwa
uchunguzi wa awali.
Kauli
ya Mmari ameitoa wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa takukuru kwa
kipindi cha robo mwaka cha mwezi Januari hadi Machi mwaka huu.
Alisema
kuwa malalamiko matano yaliyoshindwa kuthibitisha makosa ya rushwa yamefungwa
na imewafikisha mahakamani watuhumiwa wanne wa makosa mbalimbli ya rushwa
katika kesi tatu zilizofikishwa mahakamani.
Alisema
kuwa idara ya afya inaongoza kwa kuwa na malalamiko saba yanahusiana na rushwa
ikifuatiwa na serikali za mitaa katika kata na vijiji ambapo malalamiko
yaliyojitokeza ni sita.
Amezitaja
idara nyingine ambazo zina malalamiko mengi kuwa ni serikali za mitaa
kitengo cha elimu ambapo walipata malalamiko matatu, kilimo na ushirika
yalijitokeza malalamiko mawili sambamba na baraza la ardhi na sekta
binafsi waliyapata malalamiko mawili.
Alisema
kuwa idara ya polisi,mahakama na wakala wa serikali upande wa Tanroads
wamepokea lalamiko moja kwa kila idara kwa kipindi cha robo mwaka cha
January hadi Machi mwaka huu.
Hata
hivyo ameongeza kuwa taasisi hiyo imeweka mkakati wa kuwafikia wananchi wengi
zaidi ili kutoa elimu ya rushwa na kuwataka wananchi wasisite kutoa taarifa ya
rushwa kwa taasisi hiyo ili iweze kufanyiwa kazi.
0 comments:
Post a Comment