Wananchi
wa Tanzania wametakiwa kuchangamkia nafasi za kufanya baishara zilizopo
kwa nchi za Afrika Mashariki kutokana na kuwepo makubaliano ambayo
yanawapa wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kufanya biashara kwa
uhuru.
Hayo yalisemwa jana na Mbuge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere ambaye alidai
kuwa nchi za Afrika Mashariki zinashirikiana kwa mambo mbalimbali
ikiwepo umoja wa forodha, soko la pamoja, umoja wa fedha na shirikisho
wa kisiasa.
Alisema
kupitia makubaliano hayo Watanzania wana nafasi ya kwenda kufanya
baishara katika nchi zingine bila kuzuiliwa na hivyo kuwa na nafasi ya
kusambaza bishaa zao katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
“Huu
ni muda wa Watanzania kuchangamkia nafasi zilizopo za kufanya baishara
kwa nchi za Afrika Mashariki, vikwazo zilivyopo kwa sasa ni wananchi
wengi wa Afrika Mashariki bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu hilo
lakini tumejipanga katika hilo,” alisema Nyerere.
Alisema
kwa kutambua changamoto hiyo ya wananchi wengi kutokufahamu nafasi
hiyo, wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania wataendesha
programu ya kuwaelimisha Watanzania jinsi wanavyoweza kunufaika na
ushirikiano huo.
Alisema
programu hiyo ilianza Aprili 4 na itafanyika hadi Aprili, 23 ambapo kwa
kuanza wamepanga kukutana na Kamati za Bunge, Taasisi za Elimu ya Juu,
vyombo vya habari, kutembelea soko la Kariakoo na soko la Samaki la
Feri.
Pia Nyerere aliwataka
Watanzania kuwa na mazoea ya kutafuta taarifa mbalimbali kupitia
mitandao kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kukutana na fursa nyingi
ambazo hawakuwa wakizifahamu awali.
0 comments:
Post a Comment