Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akikabidhiwa baiskeli walizopewa na JSI akiwa pamoja na mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa vijijini Steven Mhapa pamoja na mkurugenzi wa halmashauri hiyo
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akikabidhiwa makabati ya ofisini waliyopewa na JSI akiwa pamoja na mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa vijijini Steven Mhapa pamoja na mkurugenzi wa halmashauri hiyo
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa watendaji wa wilaya hiyo waliopewa vifaa hivyo na mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa vijijini Steven Mhapa pamoja na mkurugenzi wa halmashauri hiyo
Na Fredy Mgunda,Iringa.
HALMASHAURI ya wilaya ya Iringa
vijijini imepokea msaada wa baiskeli na makabati kumi na moja kutoka kwa Wadau
wa malezi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (JSI) kwa ajili ya
maafisa watendaji wa ustawi wa jamii kwa lengo la kuwafikia watoto na
kufanikiwa kusaidia kutatua kero zinazowakabili watoto wanaoishi kwenye
mazingira magumu katika wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa kupokea
msaada huo,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa anawashukuru
JSI kwa msaada huo ambao utawasaidia watendaji wa halmashauri kufanya kazi kwa
ufanisi licha kuwa bado kuna changamoto nyingi katika eneo hilo.
“Msaada huu mtu anaweza ona
kama kitu kidogo sana ila unamaana kweli katika mazingira ambayo hawa watendaji
wetu wanafanyia kazi hivyo nashukuru sana kwa kutuweza kuwatumikia vilivyo
watoto wanaoishi katika mazingira magumu mungu awabariki” alisema Kasesela
Kasesela alisema mfumo huu ni muhimu kwani utawezesha kuweka taratibu za utoaji wa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na si kila taasisi ama mdau kuwa na utaratibu wake jambo ambalo lilikuwa likisababisha baadhi ya watoto kukosa huduma kutokana na sababu mbalimbali.
Pia Mfumo huu utahamasisha ushirikiano wa karibu kati ya wadau na taasisi zinazojihusisha na kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Aidha Kasesela watoa huduma kwa
watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanatakiwa kutoa huduma kwa uweledi
mkubwa kwani kazi hii ni ya kujitolea,kwa hiyo kwa wale wote watakaopata
mafunzo kwa ajili ya huduma hiyo katika Mitaa mbalimbali wawe waadilifu kwa
watoto na pia kutoa huduma bila ubaguzi kwa watoto wala kutowadhuru watoto hao
walio katika mazingira magumu.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya
Iringa vijijini Steven Mhapa aliwashukuru JSI kwa msaada uliotolewa kwa
wafanyaka wa halmashuri kwa kuwa utasaidia kutatua kwa haraka kero za watoto na
kuokoa maisha yao.
“Mimi nimefarijika kuona
mnatukumbuka maana msaada huo ni mkubwa sana kwetu ndio maana unatuona hapa
tunafuraha sana naomba tutumie salamu kwa mkurugenzi kuwashukuru sana” alisema
Mhapa
0 comments:
Post a Comment